Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limezindua kampeni ya ukaguzi wa vyombo vyote vya moto nchini yakiwemo magari, bajaji na pikipiki ili kuhakiki usalama wa vyombo hivyo.
Aidha amewataka Makamanda wa mikoa wa vikosi vya usalama barabarani nchi nzima kutenga maeneo maalum ya kufanya ukaguzi huo katika mikoa yao na kuhakikisha kila gari, pikipiki na bajaji zinakaguliwa.
Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya ukaguzi huo kufanyika katika vyombo hivyo vya moto jeshi hilo litabandika stika maalum kwenye vyombo hivyo ambapo kwa gari za biashara watalipa shilingi 7000, gari za kawaida zisizo za biashara (binafsi) shilingi 5000 ambapo pikipiki na bajaji zitachangia shilingi 2000 kama gharama za stika hizo.
Amesema kuwa, endapo baada ya kumalizika kwa kipindi cha ukaguzi huo na kubainika kuwepo kwa vyombo vya usafiri ambavyo havina stika ya ukaguzi jeshi hilo litachukua hatua za kisheria dhidi ya wenye vyombo hivyo ikiwemo kukamatwa na kuondolewa barabarani.
Ameongeza kuwa, kazi ya jeshi hilo ni kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unalindwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vyombo vya moto vinavyozingatia ubora

Comments
Post a Comment