Na WAF- DSM Serikali ya Tanzania na Banki kuu ya Dunia zimesaini mkopo nafuu utaosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuboresha huduma za dharura, kuboresha rasilimali watu katika Sekta ya afya, kuboresha utendaji na ufanisi kwenye ngazi ya zahanati. Hafla hiyo fupi imeongozwa na Waziri wa fedha na mipango nchini Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya bara Dkt. Godwin Mollel aliyemwakilisha Waziri wa Afya pamoja na mwakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Amur Mohamed na viongozi wengine kutoka Wizara ya fedha, Maji na Wizara ya Afya. Dkt. Mwigulu amesema, mpango huu nafuu, ni mwendelezo wa miradi iliyopita ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwemo kuboresha afya ya mama na mtoto hususan huduma katika ngazi ya zahanati ambapo idadi kubwa ya wananchi huenda kupata huduma. Nae, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, Wizara ya afya kwa kushirikiana na OR ...