UWT KUNDUCHI WAFANYA USAFI SHULE YA MTONGANI NA MTAKUJA
Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam
UWT Kata ya Kunduchi wametembelea shule za Msingi Mtaa wa Mtongani, Shule ya Mtongani na shule ya Mtakuja kwa dhumuni la kufanya usafi katika vyoo vya wanafunzi sambamba na Kubaini changamoto mbalimbali zinazowakumba wanafunzi na Walimu katika shule hizo zenye wanafunzi wasio Pungua 1900 Kila moja.
Akizungumza na mtandao wa HPMedia,Mwenyekiti wa UWT (K) Kunduchi Twilumba Balama amesema hatua hiyo imekuja ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 46 kuzaliwa Ccm yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja feb 5, 2023 jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kufanya usafi kama vile brashi, Fagio za brashi, detol, sabuni za kufanyia usafi, sabuni za kunawa mikono, vikombe vya maji, madumu ya maji n.k
Aidha, amesema shughuli hiyo imefanywa kwa ushirikiano wa UWT Kata ya Kunduchi pamoja na matawi yake waliambatana na Bwana Afya wa Kata Mr Adam pamoja na Katibu wa CCM Kata ya Kunduchi Donatus Kechegwa.
Hata hivyo, amewataka viongozi wote wa matawi ya Kata ya Kunduchi kufanya ziara za kushtukiza kwenye shule za serikali ndani ya matawi yao kujionea na kujiridhisha na hali ya usafi wa vyoo vya wanafunzi sambamba na kutoa elimu ya usafi kwa watoto.
Sambamba na hayo uongozi wa shule zote mbili walishukuru ujio wa viongozi hao wa UWT pamoja na kuzungumza na kushauriana namna ya kutatua changamoto zinazowakabili shuleni hususani eneo la vyoo, ambapo kamati nzima ya utekelezaji wameahidi kuhakikisha wanapata suluhisho la kudumu kwa ajili ya usafi na Afya ya watoto katika shule hizo.
Pia waliwapongeza walimu wa shule ya Msingi ya Mtakuja kwa kuanzisha club ya Afya ambayo wanatengeneza bidhaa zao wenyewe yaani sabuni kwa ajili ya kuhakikisha mazingira ya vyoo na madarasa yanakuwa katika hali ya usafi.
Pamoja na ziara hiyo katika shule hizo mbili, Katibu wa CCM Kata ya Kunduchi alitoa maelekezo kwa Afisa afya kufuatilia shule zote ndani ya Kata ya kunduchi kwenye suala zima la usafi wa shule na hasa vyoo.





Comments
Post a Comment