UDOM YAJA KIVINGINE
Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar
Wazazi na walezi wameshauriwa kutembelea banda la Chuo kikuu Cha Dodoma UDOM ili kuweza kujionea kozi mbalimbali zinazotolewa katika chuo hicho chenye ubora na kupata taarifa kuhusu chuo hicho ili waweze kujiunga.
Akizungumza mbele ya waziri w Elim Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano UDOM Rose Joseph amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanafunzi kujiunga na chuo hicho tangu maonyesho hayo yalipoanza July 17 mwaka huu katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar er Salaam.
"Banda letu ni kubwa tumejipanga kuna wataalamu wa kudahili wanaohitaji kujiunga kila ndaki kwa kuwatolea maelezo kwa kina zaidi mwanafunzi anapoenda kusoma aielewe kozi aliyoichagua kuisoma asijutie baadae pia tunatoa huduma ya afya kwa wazazi na wanafunzi" amesema Rose
Aidha, amesema wamefika katika maonyesho hayo kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho namna ya kuingia kwenye mfumo wa kujisajili na kujiunga na kuweza kuchagua program ambazo wanazihitaji.
Hata hivyo, amesema ni vyema wazazi na walezi pamoja na wanafunxi kufika katika banda hilo kwani hakuna kozi ambayo inafundishwa Tanzania ikakosekana chuoni hapo, hivyo wakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao wanadahili wanafunzi wanaohitaji kujiunga pia wanatoa huduma za afya bure.




Comments
Post a Comment