Waziri Ndejembi amtaka mkandarasi kukamilisha ukarabati kwa wakati bila kuongezewa muda wa mkataba Kukamilika kwake kutaongeza ufanisi wa uzalishaji na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani Na Mwandishi Wetu, Korogwe – Tanga Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini, huku Mradi wa Ukarabati wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale wilayani Korogwe, mkoani Tanga, ukifikia asilimia 83 ya utekelezaji. Akikagua maendeleo ya Mradi huo tarehe 29 Juni, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa, akisisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuongeza muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo. Waziri Ndejembi amesema kukamilika kwa ukarabati wa Kituo cha Hale kutaimarisha ufanisi wa uzalishaji wa umeme, kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani. “M...