HIFADHI YA MAGOFU YA KILWA KISIWANI YAENDELEA KUFURIKA WATALII WA NJE


 

Na. Beatus Maganja

Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara inaendelea kupokea makundi makubwa ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ambao wanafika nchini mahsusi kwa ajili ya  kutembelea hifadhi hiyo iliyosheheni utajiri wa kihistoria na maajabu ya magofu ya kale kwa shughuli za utalii.

Kwa mara nyingine ikiwa ni kundi la tatu la watalii wa nje ya bara la Africa kutembelea hifadhi hiyo katika kipindi cha mwezi Februari pekee,  Februari 07, 2024  ilipokea tena watalii wapatao 102 kutoka uingereza wakiwa na meli iitwayo The Hebridean Sky  ambapo  Kampuni ya kitalii iitwayo Takimis Holidays Ltd iliratibu  safari hiyo.

TAWA inaendelea kunufaika na matokeo chanya ya filamu maarufu iitwayo Tanzania The Royal Tour iliyochezwa na muongoza watalii namba moja Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupokea makundi ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali Duniani katika hifadhi  zilizo chini ya usimamizi wake.



Comments

Popular posts from this blog

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025