DC MPOGOLO AKABIDHI VIFAA VYA KUPIMIA WATOTO UREFU NA BAJAJI HOSPITAL ZA ILALA

 

Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

Serikali imesema itaendelea kuboresha vituo vya afya na kujenga vituo vipya maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hizo kwa ukaribu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Edward Mpogolo  katika hafla ya ugawaji bajaji 18  na vibao vya kupima Urefu watoto  walio chini ya umri wa miaka mitano lemgo ikiwa ni kuhakikisha wanapata takwimu sahihi katika utekelezaji na utoaji wa lishe bora.

"Vipimo hivi vitakwenda kusaidia kujua mtoto kuanzia anapozaliwa je yuko na uzito unaostahili ili aweze kusaidiwa kwenye eneo hilo, fedha zilizotengwa ni zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zinaenda kwenye afua za lishe na miongoni mwa fedha hizo milioni 22 zimekwenda  kununua vipimo hivi kwa ajili ya watoto" amesema Dc Mpogolo.

Amesema kuwa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeahidi kuboresha huduma za afya na moja ya maboresho ni eneo la ujenzi wa miundombinu ambapo Rais Dkt Samia ametenga zaidi ya Dolla bilioni 26 kuboresha miundombinu.

 Ameongeza kuwa, katika halmashauri ya jiji la Ilala na  ametoa  fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vikubwa viwili vya afya  cha Mchikichini kinachogharimu kiasi cha fedha bilion 5 na kituo cha Mzinga mradi wenye thamani ya  bilioni 2.5 na na hadi sasa kuna  vituo vya afya zaidi ya 10 na vipo katika hatua za mwisho kukamilika .

Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Dkt Zaituni Hamza amesema bajaji hizo zilizotolewa zitakwenda kusaidia katika uboreshaji wa huduma za afya kwani zitasaidia kuwafikia walengwa kwa urahisi sana.

"Tunashukuru sana Serikali chini ya Rais Dkt Samia kwa kuweka kipaumbele katika sekta ya afya, kwani ugawaji wa vipimo hivi vitakwenda kutoa takwimu sahihi kwa watoto chini ya miaka mitano "amesema Dkt Zaitun.

Ameongeza kuwa, moja ya shughuli zao ni kutekeleza vipaumbele muhimu vya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuhakikisha huduma za afya zinatolewa vizuri

"Tulitengewa fedha na katika fedha hizo hivyo  tumenunua  bajaji 18, ztakazotumika na watumishi ikiwemo 3kufutilia makuzi ya mtoto nyumba kwa nyumba ,3 chanjo,3 shughuli za kutokomeza Malaria Nchini ,3ustawi wa jamii '"amebainisha Dkt Zaituni.

Aidha watumishi wote waliokabidhiwa vifaa hivyo wameombwa kuvitunza vizuri na kuvitumia kwa mlengo uliokusudiwa.




Comments

Popular posts from this blog

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025