TMA YASHIRIKI KUTOA ELIMU YA SAYANSI YA HALI YA HEWA


Na Mwandishi wetu,

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a ameshiriki katika utoaji wa elimu ya sayansi ya hali ya hewa kwenye maonesho ya NaneNane 2024 katika. Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.

Dkt.Chang'a aliungana na wataalam wengine wa TMA katika muendelezo wa utoaji huduma za hali ya hewa nchini.

Aidha, Dkt. Chang'a alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi.

Mamlaka inaendelea kuwakaribisha wananchi wote Karibuni kwenye banda la TMA, NaneNane Kitaifa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025