WAKILI ALFRED TUKIKO AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KIVULE


Na Mwandishi wetu 

MWENYEKITI Mstaafu wa Umoja wa Vijana Chama cha Chama cha Mapinduzi (CCM)Willayani Ilala,pia ni Wakili Alfred Tukiko  Oktchi, amerudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Kivule kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wakili Tukiko amerudisha fomu hiyo makao Makuu ya ccm Wilaya ya Ilala Dar es salaam na kupokelewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Sylvester Yeredi 

Tukiko amesema yeye ni kada wa Chama cha Mapinduzi amelelewa na UVCCM mpaka amekuwa Mwenyekiti wa wilaya ana uwezo mkubwa kwa ajili ya kazi za chama.

"Nimekuwa kiongozi nafasi mbali mbalimbali  amejipima na kuona anatosha kuwaogoza wananchi wa Kivule ili ni Jimbo Jipya niweze kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo "amesema Tukiko. 

Wakili Tukiko amesema anazijua chagamoto zinazowakumba wakazi wa kivule na kusisitiza kuwa yeye ni mtu sahihi kwa Maendeleo ya wanakivule .

Amesema chama chake kikimpa ridhaa mara baada ya kupata madaraka atawatumikia na kuleta huduma za jamii ili kutatua changamoto zao 

Comments

Popular posts from this blog

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025