IZO BATTERY YAZUA GUMZO SOKONI BAADA YA UZINDUZI
Ayra Nwestz
Ikiwa ni wiki chache tangu kuzinduliwa kwa betri ya Izo betry kutoka kampuni ya Izo betri imeelezwa kuwa betri za "IZO Battery" zimezua gumzo kubwa sokoni kutokana na muitikio mkubwa wa wateja.
Kampuni hiyo imesema wateja wameipokea bidhaa yake kwa mikono miwili kutokana na ubora na uimara wake, jambo lililofikia hatua ya uzalishaji kuzidiwa na mahitaji katika soko.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Izo Mahenge amesema ujio wa bidhaa hiyo umeleta mageuzi makubwa katika soko la betrii ambapo ikiwa na sifa kubwa ya kutunza moto kwa muda mrefu.
"Sifa kubwa ya betri hii ni kutunza moto kwa muda mkubwa, ambapo sifa hiyo imeifanya betri yetu kuwa rahisi kutumia na kushika soko, haina usumbufu na kupendwa sana na wateja, ndio maana kwa sasa tuna mahitaji makubwa sana sokoni," amesema Izo
Ameongeza kuwa, ili kukabiliana na uhitaji kuwa mkubwa katika soko, kampuni hiyo imesema imepanua huduma zake kwa kuwa na mawakala zaidi ya 50 katika mikoa mbalimbali nchini lengo ni kuwafikia wateja wengi zaidi, hasa wale wa mikoani.
Hata hivyo, betri za IZO zinatumika katika matumizi mbalimbali, kuanzia mifumo ya solar hadi magari ambapo mpaka sasa bidhaa hiyo imefanikiwa kufika zaidi katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Shinyanga na hata kuvuka mipaka hadi Zambia.
Ameongeza kuwa, licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa katika soko la bidhaa hiyo lakini kampuni hiyo imesisitiza kukidhi vigezo na kupelekea kushika soko kwa muda mfupi tangu kuzinduliwa kwake hasa katika maeneo maeneo ya mikoani.
Amesema kuwa, kampuni hiyo, fursa bado ipo kwa wateja wa mikoani kupata betri hizo kupitia mawakala wake, huku ikiendelea kuboresha uzalishaji ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.



Comments
Post a Comment