LISSA LUXURY HAIR YAZINDULIWA DAR

 





Ayra Newstz

Chuo cha urembo cha Lissa College leo kimezindua bidhaa yake mpya ya nywele inayojulikana kama (Lissa luxury hair) ambayo itashika soko la urembo kutokana na ubora wa bidhaa hiyo huku bei yake ikiwa rafiki kwa kila mtanzania.

Akizungumzia na waandishi wa Habari  Jijini Dar es salaam Mkurugenzi na mmiliki wa chuo hicho, Lissa Leonce amesema kuwa wamekuja na bidhaa hiyo baada ya kufanya utafiti wa kina wa soko la bidhaa za nywele hapa nchini na kuamini kuwa bidhaa yao itashika soko la urembo.

"Tumefanya utafiti wa kina wa soko la bidhaa za nywele nchini kwetu na tumegundua kuwa bidhaa yetu itashika soko la urembo kutokana na ubora wake amesema Lissa.

Amesema kuwa maono ya chuo hicho ni kwamba, watazidi kubuni bidhaa za nywele ambazo zitaendana na uhalisia wa waafrika na zenye muonekano wa asili ambapo pia zitakuwa na bei ambazo kila mtanzania ataweza kuzimudu.

Aidha, chuo hicho pia kimemtambulisha Pinela Justine pamoja na mwanahabari Maimatha Jesse kama mabalozi wa bidhaa hiyo mpya ya nywele ambao watazunguka kufanya kampeni ya kutangaza bidhaa hiyo kote nchini.

Aidha ameongeza kuwa kupitia bidhaa hiyo mpya ambayo itapatikana maduka yote kote nchini na vyuo vyote vya Lissa itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara ambapo pia watatangaziwa biashara zao bure kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema watatoa mkono wa shukrani kwa mama wachungaji hamsini (50) kwa kuwafuata popote walipo na kuwasuka nywele sambamba na kuwatengeneza kucha bila malipo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

WANANCHI WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAONESHO YA MUHARRAM EXPO 2025