SERIKALI YAJA NA MKAKATI HUU KATIKA KUONGEZA VIRUTUBISHI KWENYE VYAKULA
Ayra Nwestz
Katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama katika kula vyakula vilivoongezwa virutubishi, Serikali imejipanga kuwafikiwa wakulima wa vijijini ambao wanatumia mashine za kusagia unga wa mahindi ambazo hazijawekewe madini wala vitamini ili kumlinda mlaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika mkutano wa 40 wa jukwaa la wadau wa urutubishaji vyakula, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Luitfrid Nnally amesema Serikali imejipanga kuwafikia watu wa vijijini katika halmashauri mbalimbali kupitia Wizara ya afya na Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo wameshaanza kuwapelekea mashine ambazo zinaweza zikaongeza virutubishi kwenye vyakula vyao.
Ameongeza pia kwa kutumia utaratibu wa usimamizi wa huduma za lishe kwenye mamlaka za Serikali za mitaa kwenye halmashauri zao mama lishe wananunua virutubishi na kuvisambaza kwa wasindikaji ambao hawafungashi huku tukiendelea kuwasimamia kisheria.
"Miaka ya nyuma tulikua tunaagiza virutubishi vya kuongeza kutoka nje ya nchi lakini kupitia Wizara ya viwanda na Biashara na maelekezo ya Rais sasa hivi tuna kiwanda ndani ya nchi ambacho kinazalisha vitamini na madini hali ambayo imeleta kuweza kufikisha huduma hiyo kwenye maeneo yote nchini"amesema
Amesema kuwa wanaendelea kuhakikisha kwamba halmashauri zinaanza kuweka nguvu kubwa zaidi kuyafikia yale maeneo ya pembezoni ambao wanajitegemea kwa chakula moja kwa moja ambao hawanunui vyakula vile ambavyo vinafungashwa mara kwa mara kwani wakulima wana mahindi yao hivyo hawaoni umuhimu wa kununua vyakula vilivyofungwa kwenye mifuko.
Kwa upande wake Mwenyekiti Baraza la Urutubishaji nchini, Gwao Omar Gwao amesema leo wamekutana wadau mbalimbali wakiwemo wa sekta binafsi na umma kujadili changamoto mbalimbali na fursa zilizopo katika kutekeleza mpango mkakati wa urutubishaji kwenye vyakula.
Amesema kuwa, suala la urutubishaji katika vyakula ikiwemo unga wa ngano, mahindi mafuta ya kula pamoja na chunvi ni muhimu sana ili kulinda afya ya mlaji hususani mama wajawazito ili kuepusha athari za magonjwa kwa watoto wanaozaliwa ikiwemo Kichwa kujaa maji, mgongo wazi na mdomo sungura.
"Mwaka 2013 Baraza hili kwa kushirikiana na Serikali tulizindua mpango maalum wa kitaifa na chini ya Rais wa kipindi hicho Dr Jakaya Mrisho Kikwete tulizindua hii kampeni ya nchini kwa bidhaa hizi mpya tatu ambazo zinaongezwa ambazo unga wa mahindi, ngano lakini pia mafuta ya kula ili kuhakikisha kwamba tunaweka virusi mahususi kwa ajili ya kupambana na matatizo mbalimbali ikiwemo upungufu wa damu"
Aidha, amesema kuwa Taasisi hiyo imelenga kuongeza Virutubishi kwenye baadhi ya vyakula ikiwemo Unga wa Mahindi, ngano, mafuta ya kula na chunvi lengo ikiwa ni kuifikia jamii kwa ukubwa zaidi ili kuwalinda na athari zinazoweza kuwapata endapo watatumia vyakula ambavyo havijaongezwa virutubishi.
"Tunalenga kuongeza Virutubishi kwenye Vyakula vya Mahindi,ambapo hadi sasa mikoa 26 Tayari imeanza kutekeleza Mpango huu "Amesema Mwenyekiti wa Baraza la Urutubishaji Nchini Gwao Omar Gwao.
Gwao Aliongeza kuwa Zaidi ya Wilaya 170 zipokatika mpango huu wa Urutubishaji.
Naye, MkurugenziTaasisi ya Mwanangu Development Tanzania(Mwadeta) Walter Miya amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wazazi waliopata watoto wenye matatizo ya Vichwa Vikubwa na mgongo wazi.
Miya amesema kuwa Endapo kutatolewa elimu ya uongezaji wa virutubishi kwenye vyakula kutawezesha kutokomeza tatizo hilo.
"Katika ukanda wa ziwa Victoria zaidi watu 700 kwa mwaka, wanakabiliwa na changamoto ya mgongo wazi na Vichwa Vikubwa amesema Walter Miya.





Comments
Post a Comment