Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2026

ZAI FOUNDATION YATOA AJIRA KWA VIJANA WA KEKO, YAPANGA KUPANUA HUDUMA AFRIKA

 Na Mwandishi Wetu  Wakati changamoto ya ukosefu wa ajira ikiendelea kuwaathiri vijana wengi nchini, Zain Foundation imeanza kuonekana kuwa chanzo cha matumaini kwa wakazi wa Kata ya Keko, wilayani Temeke, baada ya kuanza kutoa ajira na kuendesha programu za kuwawezesha vijana kujitegemea kiuchumi. Akizungumza kuhusu shughuli za taasisi hiyo, Diwani wa Kata ya Keko na mmiliki wa kampuni ya Zain, Ismaili Said Amanzi, amesema tangu kuzinduliwa kwa Zain Foundation tayari vijana 10 wameajiriwa moja kwa moja, huku wengine wakinufaika kupitia programu mbalimbali za ukuzaji wa vipaji na ujasiriamali. Amesema dhamira ya kuanzisha taasisi hiyo ni kuhakikisha vijana wanapata fursa za kujiajiri na kuendesha maisha yao bila kutegemea wengine. "Lengo letu ni kuwainua vijana wa Keko na kuwafanya wajitegemee kiuchumi. Tunataka watoke kwenye utegemezi na waweze kujenga maisha yao kupitia kazi na vipaji walivyonavyo," amesema. Kwa mujibu wa Amanzi, Zain Foundation ilianza Keko kwa makusudi il...

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24, zijazo

 

MUHIMBILI, MEGA WE CARE YAWAFUATA WANANCHI HUDUMA ZA UCHUNGUZI, CHANJO YA HOMA YA INI BURE

  Na Ayra Newstz  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imeanzisha kampeni maalumu ya siku mbili ya kutoa huduma za uchunguzi, chanjo na elimu kuhusu ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis), huku ikionya kuwa wagonjwa wengi hufika hospitalini baada ya ugonjwa kufikia hatua za hatari. Kampeni hiyo, inayofanyika kwa ushirikiano na Mega We Care Tanzania Limited,ambapo imeanza Julai 28 na itahitimishwa Julai 29, 2026 katika IDC Clinic iliyopo karibu na Kituo cha Reli ya Kisasa (SGR) katikati ya Jiji la Dar es Salaam, huduma zote zinatolewa bila malipo kwa wananchi. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Ini wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Swaleh Kitabu Pazi, alisema hatua ya kupeleka huduma katikati ya jiji imelenga kuwafikia wananchi ambao mara nyingi hushindwa kufika hospitalini kutokana na majukumu yao ya kila siku. Amesema kuwa, kliniki ya homa ya ini ya Muhimbili kwa sasa inawahudumia wagonjwa wapatao 5,000 waliosajiliwa, huku zaidi ...

VITUMBUA FESTIVAL YAZINDULIWA, WASHINDI KUNUFAIKA NA KIWANJA NA FEDHA TASLIMU

Ayra Newstz  Umoja wa Mama na Baba Lishe Tanzania (UMALITA) umetangaza kuanzisha tamasha jipya la Vitumbua Festival, litakalofanyika Julai 30, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuinua hadhi ya wachoma vitumbua, kuongeza thamani ya biashara hiyo na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa UMALITA Taifa, Avijawa Omary  alisema tamasha hilo litawakutanisha wachoma vitumbua kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano yatakayolenga kutambua ubunifu na kuwapa motisha wajasiriamali hao. Alisema mshindi wa kwanza atajishindia fedha taslimu, kiwanja pamoja na eneo maalumu la kufanyia biashara ya vitumbua, huku washindi wa pili na wa tatu wakipatiwa fedha taslimu, vifaa vya biashara na zawadi nyingine mbalimbali. "Tunataka kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu biashara ya vitumbua kwa kutambua mchango wake katika kukuza uchumi wa familia, kuajiri vijana na wanawake pamoja...

Utabiri wa hali ya hewa kwa 24, zijazo

 

KIGOMA YATARAJIA KUNUFAIKA NA SGR, WASANII WAKUBWA WAALIKWA KUMPOKEA RAIS SAMIA

Ayra Newstz  Mbunge wa Mkoa wa Kigoma Mjini Revocatus Chipando (Baba Levo) wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora–Kigoma, itakayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo mradi huo utabadilisha sura ya uchumi wa mkoa huo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,amesema tukio hilo litawakutanisha wananchi pamoja na wasanii mbalimbali wenye asili ya Kigoma na marafiki wa mkoa huo ili kushuhudia uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kimkakati. Aidha, amewataja wasanii waliopata mwaliko kuwa ni Ali Kiba, Diamond Platnumz, Linex, Chino wanamani, Dee Voice na Shilole, akisema uwepo wao utatoa hamasa kwa wananchi kushiriki tukio hilo la kihistoria. Baba levo amesema ameandaa usafiri wa basi kwa baadhi ya wananchi wanaotaka kwenda Kigoma kushiriki hafla hiyo, huku akieleza kuwa utaratibu wa kupata tiketi utawekwa wazi kwa watakaohitaji. Amessema mradi wa SGR wa Tabora–Kigo...

RAIS DKT. MWINYI AJIONEA MAFANIKIO YA TANESCO MAONESHO YA SABASABA

Miradi mipya ya kusafirisha umeme kuimarisha upatikanaji wa umeme Zanzibar Serikali yawekeza Dola za Marekani milioni 282 kuongeza upatikanaji wa umeme na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo amejionea mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya umeme na teknolojia mbalimbali zinazolenga kuboresha huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Katika ziara hiyo iliyofanyika Julai 13, 2026, Mhe. Dkt. Mwinyi alipata fursa ya kujionea miradi ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme, teknolojia za matumizi bora ya umeme ikiwemo majiko sanifu yanayotumia umeme kwa ufanisi, huduma ya Luku Janja pamoja na mfumo wa Smart House unaomwezesha mtumiaji kufuatilia matumizi ya umeme kupitia simu ya mkononi. Akitoa maelezo k...

MKURUGENZI MKUU REA APOKEA TUZO YA USHINDI WA REA SABASABA 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, leo Julai 14, 2026, amepokea tuzo ya Muoneshaji Bora wa Taasisi za Serikali (Government Institutions Exhibitor), ambayo REA ilitwaa katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026. Tuzo hiyo imewasilishwa kwake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Bi. Martha Chassama, kwa niaba ya watumishi walioshiriki katika maonesho hayo. Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mha. Saidy amewapongeza watumishi wa Wakala kwa juhudi, kujituma na ushirikiano wao ulioiwezesha REA kutwaa tuzo hiyo. Aidha, amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ushirikiano katika kutekeleza miradi ya REA vijijini na vitongojini, ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma za nishati na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

UBUNIFU WA BANDA WAIVUSHA TBA KWENYE TUZO ZA SABASABA

Ayra news  Jitihada za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuonesha fursa za uwekezaji na miradi yake ya kimkakati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), zimezaa matunda baada ya taasisi hiyo kutwaa tuzo ya mshindi wa pili katika kipengele cha Banda Bora upande wa Sekta ya Miliki na Real Estate. Tuzo hiyo ilikabidhiwa wakati wa sherehe za kufunga maonesho hayo zilizofanyika Julai 13, 2026, na kupokewa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TBA,  Amina Lumuli, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Arch. Daud W. Kondoro. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Lumuli alisema mafanikio hayo yanadhihirisha namna TBA ilivyoweza kutumia maonesho hayo kuwasogezea wananchi huduma, kutoa elimu kuhusu majukumu yake na kufungua milango ya fursa kwa wawekezaji kupitia miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP). Alisema banda la TBA lilikuwa kivutio kwa wageni wengi waliotembelea maonesho hayo kutokana na maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nch...

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo

 

JAB YAZINDUA RASMI MWONGOZO WA KISHERIA WA UTOAJI WA ITHIBATI YA MAISHA KWA WAANDISHI WA HABARI WAKONGWE

  Na Mwandishi Wetu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa Kisheria wa Utoaji wa Ithibati ya Maisha kwa Waandishi wa Habari Wakongwe, hatua inayolenga kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu na kwa utumishi uliotukuka katika maendeleo ya sekta ya habari nchini. Uzinduzi huo umefanyika leo, Julai 11, 2026, wakati wa maadhimisho ya JAB Day yaliyofanyika katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Kupitia hotuba yake iliyosomwa na Dkt. Egbert Mkoko, Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Bw. Tido Mhando, alisema mwongozo huo umeandaliwa kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa Bodi chini ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 pamoja na Kanuni zake, ili kuweka utaratibu wa utoaji wa Ithibati ya Maisha kwa waandishi wa habari wakongwe waliotoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya taaluma hiyo. Alis...

TAMISEMI : ONE STOP CENTER YATATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI SABASABA

  Ayara Newstz  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif, amesema mfumo wa One Stop Center ulioanzishwa katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) umeongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa kuwawezesha wananchi kupata huduma na ufumbuzi wa changamoto zao sehemu moja. Dkt. Seif amesema hayo, baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, akieleza kuwa mfumo huo umeondoa ulazima wa wananchi kutembelea halmashauri na taasisi mbalimbali kufuatilia huduma zinazotolewa na TAMISEMI. "Ndani ya banda moja mwananchi anapata huduma nyingi kwa wakati mmoja. badala ya kwenda halmashauri moja hadi nyingine au ofisi mbalimbali, hapa anapata maelezo, ufumbuzi wa changamoto zake na, pale inapohitajika, anaunganishwa moja kwa moja na wataalamu waliopo katika maeneo husika," amesema. Amesema wataalamu kutoka idara na taasisi mbalimbali za TAMISEMI wanatoa ushauri na ufafan...

BOT YAFICHUA SABABU ZA KUENDELEA NA RIBA YA ASILIMIA 6.25

Na Ayra Newstz  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba, amesema uamuzi wa benki hiyo kuendelea na kiwango cha riba ya sera cha asilimia 6.25 unalenga kudhibiti mfumuko wa bei, kuhakikisha benki zinaendelea kuwa na ukwasi wa kutosha kutoa mikopo na kuimarisha utulivu wa uchumi nchini. Akizungumza alipotembelea banda la BOT katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tutuba alisema kiwango hicho kilifikiwa baada ya tathmini ya hali ya uchumi wa ndani na mwenendo wa uchumi wa dunia. Alisema BOT inaendelea kulenga kuhakikisha mfumuko wa bei unabaki ndani ya kiwango cha asilimia tatu hadi tano, huku ukwasi ukiendelea kuwepo katika mfumo wa benki ili kuwezesha ukuaji wa mikopo na shughuli za kiuchumi. "Tunaamini kiwango hiki kitaendelea kuleta utulivu wa bei na kuhakikisha fedha zinapatikana kwa kiwango kinachohitajika kuendesha shughuli za uchumi," alisema. Tutuba alisema kipindi cha mavuno kinachokaribia kinatarajiwa kuongeza mzungu...

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Na Ayra Newstz  Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametoa wito kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri, wakieleza kuwa fedha hizo zimeendelea kubadilisha maisha ya wananchi kwa kuwawezesha kuanzisha na kukuza biashara pamoja na viwanda vidogo. Wito huo umetolewa walipotembelea Banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo pia walipongeza maandalizi ya maonesho hayo na ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania. Akizungumza katika maonesho hayo, kiongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amesema anaungana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kuwapongeza waandaaji wa maonesho hayo kwa kufanikisha tukio hilo ambalo limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji na ubunifu wa wazalishaji wa ndani. Amesema ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wa Tanzania umeongezeka kwa ki...

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo,leo Jula 9,2026

 

WAZIRI MKUU MGENI RASMI UZINDUZI WA KITABU CHA “MAMA SAMIA DOCTRINE OF LAW”

Ayra newstz Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania, TPBA, kimetangaza rasmi uzinduzi wa kitabu kipya cha “Falsafa ya Sheria ya Mama Samia” Mama Samia Doctrine of Law, sambamba na maandalizi ya Mkutano wake Mkuu wa Mwaka 2026. Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu wa Rais wa chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania TPBA, Debora Mcharo amesema kitabu hicho kinatoa mwangaza kuhusu mwelekeo na mafanikio ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Kitabu hiki ni muhimu sana kwa kila Mtanzania. Kinatueleza historia, falsafa na mafanikio ya nchi yetu chini ya uongozi wa Rais Samia. Tunawaomba wananchi wote wajitokeze kukisoma ili kuelewa vizuri mwelekeo wa nchi,”alisema Bi. Mcharo. Bi. Mcharo amebainisha kuwa uzinduzi wa kitabu hicho unatarajiwa kufanyika tarehe 10 Julai 2026, saa 2:00 asubuhi,  katika Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) na Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz...

KAPINGA AIPONGEZA NIDA

Waziri  wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga,  ameipongeza kampuni ya Nida kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaoendana na soko, huku akisisitiza kuwa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia.  Waziri Kapinga ametembelea banda la Kiwanda cha NIDA katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema ameridhishwa na ubora unaozalisha katika bidhaa.   Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Mahusiano wa NIDA, Mohamed Honelo, amesema kampuni hiyo, imejenga mnyororo kamili wa uzalishaji unaoanzia kwa kuwawezesha wakulima wa pamba, kununua mazao yao, kuyasindika kuwa nyuzi na vitambaa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya, kisha kuvipeleka NIDA Textile Mills kwa ajili ya uchapishaji kabla ya kuviuza kupitia maduka yake. Aidha, kampuni hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto ya ajira kwa kutoa ajira ...

UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WAANZA SEPTEMBA

Dar es Salaam. Serikali imesema itaanza ukaguzi wa vyama vya ushirika nchini kuanzia Septemba mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uwajibikaji, kuongeza imani ya wanachama na kuboresha utendaji wa sekta hiyo inayochangia zaidi ya Dola za Marekani bilioni mbili katika uchumi wa taifa. Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakaguzi na Wasimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Jeremia Jackson Mugeta, alisema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vinakaguliwa kwa wakati na kwa kuzingatia sheria. Alisema vyama vya ushirika vinapaswa kuandaa na kuwasilisha taarifa zao za fedha kwa ofisi za shirika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kurahisisha utekelezaji wa mpango wa ukaguzi wa mwaka wa fedha 2025/26. "Tunataka wanachama wa vyama vya ushirika waendelee kuwa na imani na vyama vyao kwa kuhakikisha fedha zinatumika kwa uwazi na taarifa za ukaguzi zinapatikana kwa wakati,...