Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 kuanzia saa 3:00 usiku wa Agosti 19, 2026, ikieleza kuwa baadhi ya maeneo nchini yanatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo, huku maeneo mengine yakitarajiwa kuwa na vipindi vya jua. Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Kagera na Mara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua. Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua. Aidha, Visiwa vya Unguja na Pemba, Kigoma, Tabora, Katavi, Manyara, Dodoma, Singida, Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Pwani ikiwemo Mafia, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe na Songwe vinatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi pamoja na vipindi vya jua. Mawimbi makubwa baharini TMA imesema upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya hadi kilomita 30 kwa saa katika Pwani yote, ukitoka Kusini...