Skip to main content

TANZANIA NA BANKI YA DUNIA ZASAINI MKOPO NAFUU WA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

 


Na WAF- DSM

Serikali ya Tanzania na Banki kuu ya Dunia zimesaini mkopo nafuu utaosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuboresha huduma za dharura, kuboresha rasilimali watu katika Sekta ya afya, kuboresha utendaji na ufanisi kwenye ngazi ya zahanati.

Hafla hiyo fupi imeongozwa na Waziri wa fedha na mipango nchini Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Afya bara Dkt. Godwin Mollel aliyemwakilisha Waziri wa Afya pamoja na mwakilishi kutoka Serikali ya Zanzibar Mhe. Amur Mohamed na viongozi wengine kutoka Wizara ya fedha, Maji na Wizara ya Afya. 

Dkt. Mwigulu amesema, mpango huu nafuu, ni mwendelezo wa miradi iliyopita ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwemo kuboresha afya ya mama na mtoto hususan huduma katika ngazi ya zahanati ambapo idadi kubwa ya wananchi huenda kupata huduma.

Nae, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, Wizara ya afya kwa kushirikiana na OR TAMISEMI kuanza kutekeleza mkakati huu wa kupambana dhidi ya vifo vya mama na mtoto kuanzia mwezi Machi 2023 mpaka mwezi Desemba 2027 ambapo dola za Kimarekani milioni 250 kama mkopo nafuu na mkopo nafuu wa dola za kimarekani milioni 25 kutoka Global facility financing.

Amesema, Dola za Marekani milioni 244 zilitolewa na Banki kuu ya Dunia kupitia mpango harakishi wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 556 katika vizazi hai 100,000 (TDHS 2015) mpaka vifo 238 katika vizazi hai 100,000 (WHO 2023).

Aidha, Dkt. Mollel ameeleza vifo vya watoto vimepungua kutoka 67 katika vizazi hai 1,000 (TDHS 2021) mpaka 43 katika vizazi hai 1,000 (TDHS 2022) sawa na asilimia 35%, ingawa hali hiyo haifanani kwenye kwa vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa, ambayo inaonesha kushuka kutoka vifo 25 kwa vizazi hai 1,000  (TDHS 2015) mpaka vifo 24 katika vizazi hai 1,000 (TDHS 2022).

Sambamba na hilo Dkt. Mollel amesema, Sekta ya afya inaendelea kutekeleza mkakati harakishi ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi  mpaka kufikia vifo 100 katika vizazi hai 100,000, na kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa 15 katika vizazi hai 1,000 mpaka kufikia mwaka 2025.

Pamoja na hayo, ameweka wazi kuwa, ili kufikia lengo hili Sekta ya afya itaendelea kuajiri Wataalamu wenye ufanisi na weledi, kujiimaarisha kwenye mafunzo wakiwa kazini kupitia Wataalamu wenye ujuzi wa kutosha katika eneo la kazi, kuboresha huduma za usingizi na upasuaji, kuongeza na kuboresha uanzishaji wa vitengo vya wa watoto njiti katika hospitali na kuimarisha usimamizi na uongozi wenye kuleta matokeo.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...