Skip to main content

ASKARI POLISI WALIPJIUNGA NA JESHI LA POLIS WATOA .SAADA

Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam 

Baadhi ya Askari Polisi aliojiunga na Jeshi la Polisi na kuhudhuria mafunzo ya awali mwaka 2000/2001 leo wametembelea Taasisi ya Saratani Ocean road na kutoa misaada kama sadaka kwa wagonjwa wanaougua maradhi ya saratani ikiwa ni namna ya kumshukuru Mungu kwa afya na uzima katika kipindi chote  cha kazi tangu walipojiunga na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya maofisa, wakaguzi na askari Polisi walipotembelea hospitalini hapo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Kamishna wa Polisi, Ramadhani Kingai amesema kwamba misaada hiyo imetokana na michango ya askari hao ambao walichanga na kununua zawadi kwa watu wenye uhitaji kama wagonjwa.

Aidha, Kamishna Kingai amesema sadaka ni jambo ambalo linatimiza maelezekezo ya Mungu kutoka katika vitabu vitakatifu kwa kuwahurumia watu wenye uhitaji hivyo wanachi watambue kwamba Askari Polisi ni miongoni mwa wanajamii ambao wanajali na kuwathamini hivyo wanawaombea wapone ili waweze kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo. 

Akiongea kwa niaba Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Saratani Ocean Road, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Mark Athumani Mseti  ameshukuru kwa misaada iliyotolewa na kwa uamuzi mzuri wa Askari hao kutembelea hospitalini hapo na kwamba hilo limeonesha kwamba Jeshi la Polisi halipo kwaajili ya kulinda raia na mali zao tuu bali hata kujali afya za raia wa Tanzania, na kuwaomba wananchi wanapotakiwa kutoa taarifa za wahalifu watoe taarifa ili Jeshi la Polisi lizidi kufanya kazi kwa ufansi zaidi.

Misaada hiyo imehusisha baadhi  ya vifaa tiba, sabuni za kufulia na kuogea, nguo, vitenge, vyandarua, miswaki, dawa za meno, kandambili, Pampas, mafuta ya kupaka na maji ya kunywa.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...