Skip to main content

BENKI YA MAENDELEO YAFUNGA MWAKA KIBABE

Na Mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam

Benki ya Maendeleo Plc imesema imepata faida mara mbili kwa mwaka 2022, ikipata shilling bill 1.3122 ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo ilipata milioni 587 ikiwa ni sawa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya faida iliyopata iliyochangiwa na kutoa mikopo ya riba nafuu,kupata wanahisa wapya,ulipaji wa gharama mbalimbali kupitia benki hiyo .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Benki wa benki ya Maendeleo Dkt Ibrahim Mwangalaba wakatib akitoa ripoti ya ufanisi na utendaji kazi wa Benki hiyo Kwa mwaka 2022 ambapo amesema benki hiyo imeweka historia yenye faida kwa Miaka 8 tangu kuanza kufanya kwake kazi mwaka 2015 .

Dkt Mwangalaba amesema  kuwa faida hiyo imetokana na ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 22 mwaka hadi mwaka kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 12.8 hadi shilingi za kitanzania Bilioni 15.6 mwaka 2022.

"Tunafurahi kuripoti matikeo mengine ya kifedha ya Mwaka thabiti yayoongeza ufaulu ambao Maendeleo benki imefanya Kwa mwaka 2022 kwani mwaka huo ilisajili ukusji  wa faida 184% na 163% mwaka kwa mwaka faida baada ya kodi pia kupata wanahisa 8%mapato ya kila hisa shilingi 50 za kitanzania huku faida ya benki kabla ya kodi kuongezeka hadi kuongezeka shilingi bilioni 2.02 kutoka shilingi milioni 710 kwa mwaka 2021,"amesema Dkt Mwangalaba

Amesema kuwa, Mapato halisi yaliongezeka kwa asilimia 31 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 7.6 mwaka 2021 hadi shilingi za kitanzania Bilioni 9.9 mwaka 2022,pamoja na biashara ya mikopo kutokana na kuimarika Kwa hali ya uchumi na kuboresha ubora wa vitabu vya mkopo kutoka mikopo chechefu asilimia 13 mwaka 2021 hadi asilimia 5.2 mwaka wa 2022.

"Amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 11 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 70 mwaka 2021 hadi shilingi za kitanzania 77 mwaka 2022 wakati mikopo na malipo ya awali kwa wateja yaliongezeka Kwa asilimia 5 kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 57 Hadi shilingi za kitanzania Bilioni 60 mwaka 2022" amesema Dkt Mwangalaba.

Hata hivyo, amesema mafanikio ya benki hiyo Kwa. mwaka 2022 ilisaidia Wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo Machinga zaidi ya 2500 Kwa kuwapatia Elimu kwanza ksha kuekopesha kupitia vikundi vyao benki ilitoa bilioni 3 hivyo na wao wamekuwa wakurejesha kwa uaminifu hivyo mwaka huu dirisha liko wazi la kukopa vigezo na masharti kuzingatiwa .

Aidha, amesema Benk hiyo ina matarajioa makubwa mno kusogeza huduma karibu na wananchi nchi mzima hivyo inatarajia kufungua tawi jipya Mbagala Jijini Dar es salaam,kuanzisha huduma za mtandao( Internet Banking) na huduma ya ulipaji na upokeaji wa malipo ( Payment Collection System) itakayotumika Kwa  ajili ya kulipa ada mashuleni pamoja na kulipa gharama za matibabu hospitalini.

"Mfumo huu unasaidia kulipa ada au malipo ya gharama za matibabu hospitalini,mfumo huu ukilipa tu taarifa zinafika sehemu husika hakuna haja ya kupeleka risiti ya malipo ,tunafanya hivi Ili kuwaondolea wazazi usumbufu wa kupeleka risiti shuleni au hospitalini" amesema Dkt Mwangalaba.

Aidha ametoa wito kwa wale wote wanaoendesha shughuli zao za kiuchumi kwa kukopa kuwa waaminifu kurejesha madeni yao kwa wakati kwani kufanya hivyo inawajengea sifa nzuri hata katika mabenki mengine kukopeshwa pale wanapokuwa na uhitaji wa kifedha

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...