Skip to main content

HAKI ELIMU YALAANI VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA WANAFUNZI

 

Na Mwandishi wetu, HPMedia,Dar es Salaam

Shirika lisilo la kiserikali la HAKI ELIMU limelaani vikali tukio la adhabu ya kikatili waliyoipata wanafunzi wawili wa shule ya msingi Majanja wilayani Kyerwa Mkoani Kagera kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Hatua imekuja mara baada  kusambaa kwa video fupi katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini ikimuonyesha Mkuu huyo wa shule Isaya Benjamin akiwacharaza bakora kwenye nyayo za miguu wanafunzi wawili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo januari 26,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Haki elimu,Dkt John Kalage amesema kuwa kitendo hicho kinakiuka siyo tu haki za watoto bali pia ni kinyume na maadili ya kazi ya ualimu na malezi bora kwa wanafunzi.

Dkt Kalage ameongeza kuwa shirika hilo linaipongeza Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda na uongozi wa mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka na za awali dhidi ya mwalimu aliyehusika na ukatili huo ikiwa ni pamoja na kumvua nafasi yake ya ualimu mkuu,kumsimamisha kazi na kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo ili hatua zaidi za kisheria zichukuliwe.

Aidha Dkt Kalage ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya hali ya ukatili nchini iliyotolewa na jeshi la polisi,visa vya ukatili kwa watoto viliongezeka kwa asilimia 25.9% kutoka visa 5,803 vilivyoripotiwa mwaka 2015 hadi visa 7,388 mwaka 2020.

"katika utafiti uliofanywa na shirika la Haki elimu mwaka 2020,takribani asilimia 87.9 ya watoto wa shule waliripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili huku asilimia 90 kati ya hao walisema ukatili wa kimwili waliofanyiwa ulitokana na adhabu za viboko zinazotolewa shuleni,huku asilimia 54.9 ya watoto walisema walimu wao na walezi wanatumia kupiga ngumi na makofi kama Sehemu ya adhabu"amesema  Dkt Kalage.

Kutokana na matukio hayo shirika hilo pia limeishauri Serikali kuchukua hatua ambazo zitakomesha kabisa matumizi ya adhabu za viboko shuleni na kuhimiza adhabu chaya/mbadala ambazo siyo za kikatili.

"Ni rai yetu vipengele vya sheria ya elimu ya mwaka 1978,mwongozo wa elimu  juu ya adhabu za viboko wa mwaka 2002 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009,vipitiwe upya ili kukataza kabisa matumizi ya viboko shuleni na kuzuia adhabu nyingine ambazo zinaweza kutoa mwanya wa ukatili wa watoto kufanyika"ameongeza Dkt Kalage.

Sambamba na hayo shirika hilo limetoa mapendekezo 9 kwa Serikali ikiwa ni pamoja na program ya uanzishwaji wa shule salama 600 nchi nzima ambayo inalenga kuondoa ukatili wa namna yoyote na kuzifanya shule kuwa Sehemu salama na rafiki pa kujifunzia ambayo imetangazwa hivi karibuni na serikali,ilenge shule zote 18,000 nchini ikiwemo shule za msingi 12,000 na sekondari 5000.

Mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na Serikali kuweka mipango endelevu ya kuimarisha mifumo rasmi ya ulinzi na usalama kwa watoto ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa madawati ya ulinzi na usalama kwa watoto shuleni pamoja na wadau kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto katika maeneo ya shule, nyumbani, nyumba za ibada na maeneo yote ambayo watoto hukusanyika.

Hata hivyo Dkt Kalage ameongeza kuwa, Haki elimu inapendekeza Serikali kuchukua hatua dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya ukatili wa dhidi ya watoto ili kuvikomesha ndani na nje ya shule pamoja na kuhuisha miiko na maadili ya walimu ili kuwagusa hata walimu ambao wanashindwa kuzuia matendo ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na walimu wenzao mashuleni kama ambavyo imeonekana katika video ya tukio la mwalimu mkuu kupitia video iliyosambaa mitandaoni.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...