Skip to main content

TANESCO YAJA NA MATUMAINI TELE KWA WANANCHI


Na mwandishi wetu HPMedia, Dar es Salaam 

Imeelezwa kuwa katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme nchini unakuwa wa kudumu, Shirika la Umeme nchini TANESCO linaendelea na ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo limefikia asilimia 80.22 hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2022.

Aidha, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kwa sasa hali ya upungufu wa umeme nchini umepungua kwa kiasi kikubwa na kufanya hali ya upatikanaji wa umeme kuboreka zaidi hivyo kupunguza adha ya mgao wa umeme uliokuwepo hapo awali.

Akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema maboresho ya upatikanaji wa umeme yametokana na mipango ya muda mfupi na wakati ambayo imekwishatekelezwa na shirika hilo pamoja na uwepo wa mvua za vuli.

Amesema kuwa,  urefu wa kina cha maji la bwawa hilo umefikia mita 126.12 kutoka usawa wa bahari na bado wanaendelea kujaza maji na linatarajiwa kujaa baada ya misimu minne ya mvua za vuli na masika na wataanzisha miradi ya vituo vipya vya kutumia gesi na umeme jadidifu.

Aidha amesema kuwa katika mipango ya muda mfupi tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba II na umeshaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia Novemba 24 /2022 pamoja na mitambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo namba III.

Hata hivyo, amesema kuwa tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha kidatu na unazalisha megawati 50 za umeme kwenye Gridi ya Taifa pamoja na ufungaji wa mitambo mitatu iliyopo katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I na kinaingiza megawati 120 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

Amesema kuwa,  licha ya upatikanaji umeme kuboreka shirika linaendelea kushuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya umeme kutoka asilimia 6 hadi 11 kwa mwaka ambapo ongezeko hilo limeshuhudiwa kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Hata hivyo, amesema kuwa mvua za vuli zilizonyesha hivi karibuni hazikuwa toshelevu kama ilivyotegemewa hivyo shirika bado litaendelea kufanya matengenezo ya mitambo yake ambayo haikufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu na watatoa taarifa kwa wateja pindi yatakapofanyika.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...