Skip to main content

TAMASHA LA PASAKA LA KUMSHUKURU MUNGU KWA UONGOZI WA RAIS DKT SAMIA YAENDELEA VIZURI

 


Na Magrethy Katengu,HPMedia, Dar 

MKURUGENZI wa Msama Promotion Alex Msama amesema maandalizi ya Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 9, 2023 viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam yanaendelea vizuri.

Msama ameyasema  hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kueleza namna maandalizi ya Tamasha hilo yalipofikia na Jumla ya wanamuziki wa nyimbo za Injili waliothibitisha kushiriki.

“Maandalizi ya Tamasha yako vizuri na tumejipanga vya kutosha  Tamasha hilo litakuwa ni lakipekee kwani ni urejeo mpya kwa sababu halijafanyika kwa takribani miaka saba (7) iliyopita hivyo watu wote wa dini zote mnaalikwa hakuna kiingilio ni buree"amesema Msama

Msama amesisitiza kuwa  lengo la Tamasha hilo ni kuwafanya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka katika mazingira mazuri na ndiyo maana wameliweka viwanja vya Leaders Club ili iwe rahisi kila mwananchi kufika.

Pia Tamasha la Pasaka litatumika kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi nzuri katika Mambo mengo ikiwemo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Chini ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia miradi yote imetekelezwa vizuri na biashara zinaenda vizuri, hivyo tunayo kila sababu ya kumshukuru Mungu katika Tamasha hili la Pasaka,” amesema Msama.

Hivyo amewehimiza wananchi hususan wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwani usalama utakuwepo wa kutosha na watapata burudani kutoka wa waimbaji wengi nguri ambao wamethibitisha kushiriki.

Baadhi ya waimbaji hao ni Joshua Ngoma kutoka Rwanda, Tumaini Akilimali kutoka Kenya na Zabroni Singers kutoka Tanzaniha.

Wengine ni Upendo Ngoma kutoka Tanzania, Upendo Nkone kutoka Tanzania, Masi Masilia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ambwene Mwasongwe kutoka Tanzania na Joshua Mlelwa kutoka Tanzania.

Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa amesema kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kwenye suala la muziki.

“Tumeshapata kampuni itakayofunga vifaa vya muziki vya kisasa,” amesema Mabisa.

Amesisitiza kwamba watafanya tamasha kubwa na lakihistoria huku wakisherehekea miaka miwili ya Rais Dkt. Samia.

Amesema kwamba wameamua kulifanya Tamasha hilo katika viwanja vya Leaders Club kwa sababu ni eneo kubwa na la wazi.

Naye Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Christopher Mwahangila amethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

Amewataka Watanzania kwa ujumla kuhudhuria kwani wamejipanga kutoa burudani nzuri kwani walikuwa wamelimisi Tamasha kwa muda mrefu.

“Mimi nimiongoni mwa waimbaji watakaoshiriki, tulikuwa tumelimisi hili Tamasha, ewe Mtanzania usikose kufika, kwani tamasha ni bure kabisa,” amesema Mwahangila.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...