Skip to main content

HII HAPA HISTORIA YA MEMBE NI BALAA

 


Bernard Kamilius Membe alizaliwa tarehe 9 Novemba, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati wa watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe.

Bernard Membe ni Mmwera, na kama ilivyo desturi ya Wamwera, watoto hutumia jina la ukoo wa Mama. Hivyo watoto wote saba wa familia hii ya Mzee Kamillius wamekuwa wanatumia jina la upande wa mama yao, Cecilia, yaani Membe.

Elimu
1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.

1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi.

1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora.

1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais.

1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika maswala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa (Bachelor Political Science and International Relations)
1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika ofisi ya rais.

1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa (Masters- Economics, International Relations and International Law).

1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi wa mambo ya ulinzi na usalama

Mafunzo
Kati ya mwaka 1975 na 1976 Ndugu Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ambapo vijana wote waliohitimu kidato cha Sita walitakiwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya Jeshi, Ndugu Membe aliajiriwa katika Ofisi ya Rais, Utawala bora.

Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza. Aidha, mwaka 1980, Ndugu Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam.

Familia
Mwaka 1986, Ndugu Bernard Membe alifunga ndoa Takatifu na Dorcas Richard Masanche, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam. Ndugu Membe na mama Dorcas wamejaliwa kupata watoto watatu, Cecilia, Richard na Denis.

Siasa
Ndugu Membe ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Kamanda wa Vijana wa Mkoa wa Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, na Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mwaka 2000, aliingia Bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Mtama, kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Licha ya uchanga wake bungeni, akiwa kama mbunge wa kawaida (back bencher), Bernard Membe alikuwa mchangiaji mkubwa wa mijadala inayohusu Amani, Ulinzi na Usalama pamoja na Utawala Bora.

Mwaka 2005, Bernard Membe alichaguliwa tena na wananchi wa Jimbo la Mtama kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Tofauti na kipindi cha nyuma, Bernard Membe alianza muhula wa pili wa Ubunge, Januari 2006, kama ‘front bencher’ baada ya kuteuliwa na rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri mnamo mwezi Oktoba, 2006, Bernard Membe alihamishwa Wizara na kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati na Madini – moja ya wizara ngumu na nyeti kwa Taifa.

Hata hivyo miezi michache baadae, yaani January 2007, rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Bernard Membe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa baada ya aliyekuwa anashikilia wadhifa huo – Dr Asha Rose Migiro – kuteuliwa na Katibu Mkuu Baraza la Umoja wa Kimataifa na kuwa Naibu Katibu mkuu wa baraza hilo.

Bernard Membe amehudu katika nafasi hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu 2007 hadi 2015, akiwa ni Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa miaka mingi mfululizo, akitanguliwa na Rais Kikwete ambaye alidumu katika Wizara hiyo kwa miaka 10 mfululizo.

Mafanikio
Bernard Membe ameongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kipindi ambacho Tanzania na dunia, kwa ujumla, ilikabiliwa na changamoto kubwa katika mambo mbalimbali yanahusiana na ulinzi na usalama, uchumi na ajira (hasa kwa vijana). Changamoto hizo zimepelekea hali ya amani kwa ujumla kutetereka katika maeneo mengi ya dunia.

Hata hivyo, chini ya uongozi wa Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa, Tanzania imeendelea kuwa mtetezi na mshirika mkubwa wa ulinzi na usalama ndani ya Ukanda wa Afrika na duniani. Tanzania imeshiriki kuleta amani katika nchi za Maziwa makuu yaani, DRC, Burundi na Malawi, lakini pia Tanzania imeshiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za Comoro, Madagasca, na Sudan ya Kusini. Aidha, Tanzania imekuwa mshiriki mzuri katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika mataifa ambayo yalipata machafuko kisiasa.

Uchumi
Bernard Membe amesimamia vema utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya uchumi ili kuwezesha Tanzania kufanya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuininua hali za wananchi wake. Ni katika kipindi chake, nchi imeshuhudia uwekezaji mkubwa katika eneo la viwanda, gesi, makaa ya mawe, kilimo na utalii. Chini ya uongozi wa Ndugu Bernard Membe, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilipata tuzo ya utendaji bora iliyotolewa na sekta binafsi kwa kutambua mchango mkubwa wa Wizara katika kukuza sekta binafsi Tanzania.

Kudumisha mahusiano kimataifa: Katika kipindi chake, Tanzania imefanikiwa kuipaisha Diplomasia yake katika Jumuiya ya Kimataifa kwa kutembelewa na viongozi mbalimbali mashuhuri kama, Marais George W. Bush na Baraka Obama wote wa Marekani, Xi Jinping wa Uchina, Joachim Gauck wa Ujerumani, Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Piere Nkuruzinza wa Burundi, Joseph Kabila wa DRC, Philipe Nyusi wa Msumbiji, Mwana wa Mfalme wa Malkia wa Uiengereza, na Mwana wa Mfalme wa Japan.

Pia chini ya uongozi Ndugu Bernard Membe Tanzania imefanikiwa kupanua wigo wa mahusiano yake Kaimataifa kwa kufunguwa Balozi mpya katika nchi za Malaysia, Brazil, Comoro, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait. Aidha, Wizara imefanikiwa kufungua upya Ubalozi wa Tanzania the Hague, Uholanzi uliofungwa mwaka 1994. Kadhalika Balozi Mpya za Brazil, Oman, Uturuki, Kuwait, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Namibia zilifunguliwa hapa nchini.

Kutambuliwa
Kwa kutambua mchango wake katika kurejesha hali ya amani na utulivu katika Visiwa vya Comoro, mwaka 2008, Bernard Membe alikuwa miongoni mwa watanzania waliotunukiwa Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro na rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Uozefu

2006 – Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.

Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC.

2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM.

2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.
2006 – Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa.

2013 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth.

2014 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amekuwa mjumbe wa kamati za usuluhishi katika migogoro kwenye nchi za Sudan ya Kusini, Madagascan na katika mzozo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Pia Tanzania imefanikiwa kushiriki katika zoezi la Uangalizi wa chaguzi kwa niaba ya SADCC katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagasca, Kenya, Comoro na Afrika ya Kusini.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...