Skip to main content

UVCCM TAIFA - "HAWANA HOFU MASHIRIKIANO YA KUIMARISHA UCHUMI WA BANDARI"

 


Na Magrethy Katengu, HPMedia, Dar 

Umoja wa  Vijana Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema Serikali inachofanya sasa ni mashirikiano ya Uwekezaji Bandarini ili kwenda kusaidia kuimarisha miundombinu ya bandari na shughuli nyingine za lojistiki na Uchukuzi ili Taifa liwe kitovu cha uchumi Imara.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Mohamed Kawaida, amesema kinachofanyika siyo maamuzi ya mtu binafsi bali ni maelekezo ya Chama kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kupitia ibara 22(1)

Aidha amesema kuwa, kupitia uwekezaji ambao utafanyika utasaidia kuondoa urasimu na dosari zinazosababisha ucheweshwaji wa utoaji mizigo Bandarini.

Hata hivyo, amesema licha ya kusambaa mizozo mitandaoni kuhusu bandari, katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 (a) inaeleza"kila mtu anao Uhuru wa kuwa na maoni ya kueleza fikra zake "hivyo wanaheshimu maoni ambayo yanatolewa na yanayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali kuhusu azimio hilo ambalo linaridhiwa na Bunge kwa mujibu ya Ibara 63-3(e) ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka Mkataba unaoingiwa na Serikali upitiwe Bungeni kabla ya kutekeleza .

"Serikali ya Tanzania imeingia Mkataba wa mashirikiano na serikali ya Dubai kwa kuanzisha Ushirikiano wa kuboresha ,kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini suala ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa serikali kufikia malengo ya kiuchumi na kijamii na majadiliano haya na maandalizi yanafanywa na Timu ya wataalamu wa Tanzania ambao Wana uzoefu mkubwa katika Masuala ya mikataba ya kinataifa na kabla ya kusainiwa ulizingatia taratibu zote za nchi yetu " amesema Kawaida

Hata hivyo, amebainisha kuwa Ushirikiano pamoja na mambo mengine unajikita kwenye maboresho uendeshaji wa shughuli za bandari nchini kwa kuongeza tija na ufanisi kusimika mfumo ya kisasa ya TEHAMA na kuwajengea uwezo kupitia mafunzo Watanzania katika uendeshaji wa shughuli za bandari kuhusu changamoto za bandari mifumo ya TEHAMA ya bandari kisasa na inayosoma na mifumo mingine ikiwemo Mamlaka ya Mapato TRA hali inayosababisha kutokuwa na udhibiti wa kutosha katika kukusanya mapata ya nchi.

Aidha amesema kuwa jitihada zote na hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya Awamu ya sita katika kuvutia uwekezaji nchini hususani kwenye maeneo ya bandari nchini  zinalenga kumalizia changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika bandari zetu ambako kumekuwa kukichangia katika sekta zingine .

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...