Skip to main content

DUMU 364 ZAKAMATWA KUNDUCHI, MITUMBWI MIWILI FERI


Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji kinaendelea na Operesheni maalum iliyoanza Julai 19, 2023 na inayoendelea katika kudhibiti uhalifu ukanda wa Bahari ya Hindi.

Aidha katika Operesheni hiyo Kikosi kazi cha Operesheni cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam wakitumia boti ya Polisi walikamata mitumbwi miwili isiyokuwa na jina wala usajili huko maeneo ya feri Wilaya ya Ilala, na Tafico Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam, iliyokuwa inatumika kuvua samaki kwa kutumia nyavu haramu aina ya kokoro.

Katika hatua nyingine, operesheni hiyo Julai 25, 2023 majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kunduchi katika bahari ya hindi askari Polisi kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato.

Nchini (TRA) wakiwa doria walifanikiwa kuwakamata Abdalla Jecha @ omary (37) na Khatibu Kombo (23) wakiwa na Jahazi liitwalo SAFINIA lisilokuwa na namba za usajili likiwa limebeba mafuta ya kupikia aina ya ACTER dumu 364 na kila moja likiwa na lita 20 yakitokea Unguja kwenda Dar es Salaam kwa kupitia bandari bubu ya kunduchi wakiwa na nia ya kukwepa ushuru wa forodha. 

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini watuhumiwa hao hawakuwa na nyaraka zinazothibitisha uhalali wa umiliki wa mizigo hiyo ya mafuta ya kupikia pamoja na nyaraka za usafirishaji. Jeshi la Polisi linawahoji watuhumiwa hao kwa kina na baadae taratibu nyingine za sheria ziweze kuchukuliwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara nyingine za serikali kuhakiki mzigo huo, pia linawapongeza wananchi wote ambao wanachukia uhalifu wa aina zote na ambao wanatoa taarifa zinazo pelekea kubaini na kuzui uhalifu.

Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa wafanyabiashara wasio na uadilifu kuacha kusafirishaji mizigo kwa njia ya bahari bila kuwa na nyaraka za mizigo hiyo, Jeshi la polisi Kikosi cha Wanamaji halitasita kuwakamata na kufikisha kwenye vyombo vya sheria na hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...