Skip to main content

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KILIMO

 

Na Mwandishiwetu, HPMedia, Dar 

Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRED Latifa Khamis amezindua kongamano la kimataifa la biashara ya mazao ya kilimo (World agrifam) ilikua lengo kuu ni kufungua fursa kwa wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde korosho mafuta pamoja na pamba kwa kwani  walaji wakubwa wa mazao hayo ni bara la Asia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua kongamano hilo wakati akimuwakilisha Waziri wa Viwanda Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa, ni jambo la kupongezwa kwa ubalozi wa India kwa kuamua kuleta kongamano hilo Nchini Tanzania kwani wakulima wadogo watapata fursa ya kuonana na wahusika wenyewe wanaojihusisha na mazao ya kilimo.

Aidha, amewataka watanzania kushiriki kwa wingi katika kongamano la kimataifa la biashara ya mazao ya kilimo World agrifam ili kuweza kupata fursa ya kuuza mazao mbali mbali nje ya nchi.

Amesema kuwa, kwa mazao ya kilimo yamekuwa yakifanya vizuri katika soko la nje hususani zao la parachichi kutoka mkoa wa  mbeya .

"Hatukutegemea kama zao la parachichi  kutoka mbeya lingeweza kufanya vizuri lakini tumeskia namna ambavyo linavyofakazi hivyo ni waombe wakulima wazidi kujitokeza ili kuweza kupata uzoefu wa kilimo"amesema Latifa .

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Pulses Network (TPN) Zirack Andrew ambaye pia ni muandaaji wa kongamano hilo  amesema mkutano huo wa mazao ya chakula unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika hususan nchini Tanzania.

Amesema kuwa, kongamano hilo limefanikiwa kuleta makampuni zaidi ya 700 kutoka nchi mbali mbali duniani kote na ni  kongamano ambalo linajumuisha mazao yote yanayolimwa afrika.

Aidha, amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni sekta ya chakula Bora kwa ajili ya ustawi wa afrika ambapo wamewakutanisha wanunuzi kutoka nje na wauzaji wa ndani ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na uwekezaji katika ongezeko la thamani .

"Bado Teknolojia yetu sio nzuri kitu ambacho mazao yetu ya chakula huuzwa chini ya kiwango hali inayopelekea bei ya chakula kuwa chini wakati tungeweza kuchakata chakula tungeweza kuuza katika thamani ya juu"amesema Andrew.

Hata hivyo, amewataka watanzania ambao bado hawakuweza kufika katika kongamano hilo ni vyema kufika katika viwanja hivyo vya diamond jublee  ili waweze kujifunza vitu mbali mbali.

Amesema kongamano hili limeanza Jana  hadi Agost  12 ambapo yatahusisha wataalam kutoka nchini India na makundi ya wakulima wa Bara la Afrika, ambapo zaidi ya watu 3000 watembelea na kushiriki maonesho haya, dhamira ni kufungua masoko ya Mazao yetu ya chakula ya Afrika Kimataifa. 

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taso Event Organizer, Suveer Rajpurohit, amesema kwamba wamekuja barani Afrika kwa ajili ya kutafiti fursa ya soko kwa mazao ya Kilimo ya Afrika na India,huku akiwakaribisha wakulima kutembelea maonesho hayo ili kuona fursa mbalimbali zitokanazo na Kilimo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...