Skip to main content

MAKONDA AWAJIA JUU TANESCO, ATOA RAI KWA WANANCHI

Na fatma Ally, Habari Plus Media

KATIBU wa Itikadi na Uenezi  Paul Makonda amelitaka shirika la umeme Tanesco kujitafakari upya kwa hali ya ukatikaji wa umeme ovyo ambapo imekua ni changamoto kubwa jambo ambalo limekua linarudisha nyuma harakati kubwa za maendeleo kwa taifa.

Kauli hiyo, ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akitoa tathmini ya robo mwaka ya chama cha mapinduzi amesema kuwa, hivi karibuni Tanesco wamemuahidi Rais Samia ya kwamba ifikapi Januari kuwa kinu cha umeme kitawashwa hivyo ni vyema ahadi hii ikatekelezwa kwa vitendo.

Aidha amewataka watendaji wote kuanzia ngazi shina hadi mkoa kusikiliza kero za wananchi Ila kutatua changamoto zinazowakabili na sio kukaa ofisini

"Nataka niwakumbushe ndugu viongozi tuliopewa dhamana na Rais Samia ya kuwatumikia wananchi ni vyema tukatekeleze wajibu wetu tusisubiri mpaka Rais Samia anzishe ziara aanze kasimamishwa njiani na wananchi ili watoe malalamiko yao"amesema Makonda.

 katika hatua nyengine amewataka wananchi  kujitokeza kwa wingi katika suala la utoaji wa maoni ya dira ya Maendeleo ya Taifa ya  miaka 30.

"Niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika suala zima la utoaji wa maoni ya nini wanachotaka kiwekwe, na mpango huu utawafikia wananchi wote kwa sababu tayari tume maalum imewekwa kwa ajili ya kukusanya maoni hayo"amesema Makond

Akizungumzia suala la kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Makonda amesema ni vyema wanachama wenye nia ya kugombea uongozi kuacha viongozi waliopo madarakani waendelee kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao bado ni viongozi halali wanaotambulika kisheria.

"Najua wapo watu ambao wameanza kampeni za hapa na pale mimi niwambie tu ndugu zangu waacheni viongozi wafanye kazi kwa sababu muda wao haujaisha na wao bado ni viongozi wanaotambulika na bado wanahaki ya kuwatumikia wananchi", amesema Makonda.

Hata hivyo Pauli Makonda  amebainisha kuwa kuanzia Januari 13 /2024 ataanza ziara ya kikazi katika mikoa 10 ikiwemo  Tanga, Pwani,Kilimanjaro,Arusha,Manyara,Singinda,Tabora,Shinyanga  na Simiu.

Aidha kupitia ziara hoyo amewataka watendaji wa halmashauri zote watakaopitiwa na ziara hiyo waanze kujitathmini kabla ya kiongozi huyo kupita maeneo hayo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...