Skip to main content

DKT. BATILDA BURIAN AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA JITAHADA ZA KUKUZA UTALII MKOANI TABORA


Na. Beatus Maganja

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa jitihada za dhati za kukuza utalii Mkoani Tabora.

Dkt. Batilda alitoa pongezi hizo Januari 15, 2024 alipotembelewa na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ofisi kwake akiwa katika ziara ya kikazi Kanda ya Magharibi iliyokuwa na lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazofanywa na TAWA Mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema anatambua jitihada zinazofanywa na TAWA katika kuboresha miundombinu ya utalii katika bustani ya Wanyamapori Mkoani humo ijulikanayo kama Tabora ZOO na kuishauri Mamlaka hiyo kuangalia uwezekano kuongeza miundombinu katika bustani hiyo kwa ajili ya kuongeza mapato.

Vilevile, alishauri kuongeza mazao mbalimbali ya wanyamapori kama vile sumu ya nyoka ambapo alisema kuwa inahitaji utafiti zaidi.

Pia Dkt. Batilda alisema ili kuendelea kuchagiza shughuli za utalii Mkoani humo, TAWA ione namna bora ya kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii ikiwemo bustani ya wanyamapori ya Tabora.

Aidha, aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAWA ili kuhakikisha shughuli za Uhifadhi na Utalii zinazofanywa na taasisi hiyo zinazidi kuimarika.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda alimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora kwa ushirikiano na mshikamano anaoutoa kwa taasisi yake anayoiongoza katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiuhifadhi na utalii Mkoani humo

Ziara ya Kamishna Mabula katika  Kanda ya Ziwa, Kati na Magharibi ililenga kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii zinazofanywa na TAWA katika Kanda hizo ikiwa ni pamoja na kukagua miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa karakana ya kutengenezea magari na mitambo Wilayani Manyoni.

Pia kuzindua jengo la ofisi ya Pori la Akiba Moyowosi Wilayani Kibondo na kutembelea familia za ndugu walioathiriwa na wanyamapori aina ya mamba na kuwapa pole katika vijiji vya Kasahunga na Mayolo wilayani Bunda

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...