Skip to main content

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UVIKO PORI LA AKIBA WAMI MBIKI

Na. Beatus Maganja

Kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi ya mpango wa Taifa wa  maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 iliyotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ndani ya Pori la Akiba Wami Mbiki Mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na  kukagua miradi hiyo,  Mwenyekiti wa Kamati  Mhe. Timotheo Mzava amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu wake wa kutafuta fedha na maelekezo aliyoyatoa juu ya matumizi ya fedha za UVIKO ambazo zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii.

"Kwa mazingira na hali tuliyoiona (Pori la Akiba Wami Mbiki) nadhani tutaungana sote kumpongeza kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye Nchi yetu lakini hasa kwa ubunifu mkubwa alionao wa kutafuta fedha lakini pia maelekezo aliyoyatoa Juu ya matumizi ya fedha za UVIKO "

Mhe. Timotheo Mzava ameelekeza pia pongezi za Kamati yake kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na TAWA kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kusimamia miradi hiyo ambayo iligharimu zaidi ya TZS bilioni mbili.

Sanjari na pongezi hizo, Kamati hiyo imetoa wito kwa TAWA kuongeza mikakati ya kibiashara na ya kimasoko ikiwa ni pamoja na kutangaza hifadhi hiyo ili miundombinu iliyotengenezwa iweze kutumika kama ilivyokusudiwa na Serikali kupata tija inayotarajiwa


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Malialisi na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inaongeza jitihada katika kutangaza hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya wageni ikiwa ni pamoja na kutafuta wabia wa kushirikiana nao katika kuendesha shughuli za utalii na uwekezaji


Awali akifafa


nua hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu mikakati ya TAWA katika kuchechemua utalii katika hifadhi ya Wami Mbiki, Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda amesema TAWA imekuja na mpango mahsusi wa kufufua hali ya hifadhi hiyo kwa kumtafuta mwekezaji ambaye atawekeza kituo cha kuokoa na kulea Wanyamapori wenye mahitaji maalumu (Wildlife Rescue and Rehabilitation Centre).

Amesema tayari TAWA imekwisha saini mkataba na mwekezaji huyo ambao unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa Wanyamapori wenye mahitaji maalumu kama vile wagonjwa, yatima, walionusurika katika matukio ya ajali na wanyamapori wanaotelekezwa na wazee wanaohitaji uangalizi maalumu.

Aidha amesema uwepo wa kituo hicho katika hifadhi ya Wami Mbiki utakuza utalii wa ndani na wa nje kupitia program mbalimbali zitakazoendeshwa ikiwemo program ya watalii wa kujitolea, utalii wa matukio lakini pia mwekezaji ameahidi kuleta wageni kati ya 30 mpaka 50 Kila mwezi jambo ambalo litachagiza utalii katika hifadhi hiyo.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na  Utalii katika ziara hiyo ni pamoja na  barabara yenye urefu wa kilometa 47.2, mabanda ya kulala wageni,  lango kuu la kuingilia wageni linalojumuisha maduka ya kuuza bidhaa za utalii (Curio shops), jengo la kupumzikia wageni, jengo la kutoa taarifa kwa wageni (Visitors' Information Center), kituo cha mauzo, vyoo pamoja na nyumba za kuishi Maafisa na Askari watakaokuwa wakihudumia wageni.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...