Skip to main content

KAMISHNA MABULA AFANYA UKAGUZI WA KARAKANA YA KISASA MANYONI, ATOA MAELEKEZO MAHSUSI


Na. Beatus Maganja 

Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ameeleza kufurahishwa kwake na ubora wa viwango vya ujenzi wa karakana ya matengenezo ya magari na mitambo iliyojengwa Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, karakana inayotajwa kuwa ni kubwa kuliko karakana zote zilizojengwa na taasisi hiyo.

Ameyasema hayo  Januari 14, 2024 akiwa katika ziara yake Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, ziara yenye lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazotekelezwa na TAWA wilayani humo.

"Nimetembelea na kukagua karakana, kimsingi nimeona imejengwa vizuri na pia nimeona ina uwekezaji mkubwa wa vifaa vitavyotumika na nina imani hii karakana itatusaidia sana" amesema

Akibainisha sababu za kuifanya karakana hiyo kuwa kubwa wilayani humo, Kamishna Mabula amesema Manyoni ni katikati ya nchi na ni sehemu inayofikika kwa urahisi, hivyo kutokana na ukubwa wake itatumika kutengeneza magari si tu ya Kanda ya Kati bali ya taasisi nzima.

Aidha, Kamishna Mabula ameuelekeza uongozi wa Kanda hiyo kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi wa karakana ikiwa ni pamoja na kuwapeleka wataalamu wa vifaa hivyo ili iweze kusimamiwa na kuendeshwa Kisasa.

Vilevile Kamishna Mabula ametumia ziara hiyo kuwahimiza Maafisa na Askari wote wa TAWA kurejea mpango mkakati wa  taasisi hiyo ambao unafikia kikomo Mwaka 2026 ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Amefafanua kuwa mpango mkakati wa TAWA una malengo makuu matatu ambayo ni kuhakikisha rasilimali ambayo TAWA imepewa kusimamia inakuwa salama, pia kuhakikisha wateja wote wa taasisi wakiwemo wawekezaji wanapata huduma na kuridhika na huduma inayotolewa na lengo la tatu ni kuhakikisha TAWA inafanya kazi kwa ufanisi na tija.

Kamishna huyo amesisitiza kuwa malengo hayo hayataweza kutimia bila kuishi  katika tunu za taasisi hiyo ambazo ni uadilifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kutenda kazi kwa ubunifu pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Naye Kamishna Msaidizi Ulinzi wa Rasilimali za Wanyamapori Hadija Malongo akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa Kanda ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TAWA kwa kuwezesha ujenzi  wa karakana hiyo ambayo kukamilika kwake kutasaidia kupunguza gharama za matengenezo ya magari ambayo ilikuwa changamoto kubwa mradi wa ujenzi wa karakana hiyo umegharimu zaidi ya TZS Million 217.




Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...