Skip to main content

KAMISHNA WA TAWA AZINDUA MRADI WA JENGO LA OFISI LENYE THAMANI YA ZAIDI YA TZS MILIONI 250, AMPONGEZA RAIS SAMIA

 

Na. Beatus Maganja 

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania - TAWA amezindua mradi wa jengo la ofisi lenye jumla ya vyumba 8 vikiwemo vyumba 6 vitakavyotumika kama ofisi, chumba cha mikutano, stoo pamoja na vyoo viwili, mradi unaotajwa kugharimu zaidi ya Tsh. Millioni 250.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa  jengo hilo iliyofanyika leo Januari 16, 2024 Makao Makuu ya Ofisi za Pori la Akiba Moyowosi zilizopo Kifura wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mabula amemshukuru Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiwezesha taasisi hiyo kukamilisha mradi huo na miradi mingine ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa TAWA.

"Tunamshukuru Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya kazi nzuri ya kutupatia fedha zilizotuwezesha kukamilisha mradi huu na miradi mingine tunayoitekeleza ikiwa ni pamoja na mishahara, yote hii ni matokeo ya Serikali yetu, ndiyo inayotuwezesha" amesema.

Aidha, Kamishna Mabula amewataka wahifadhi wa Pori la Akiba Moyowosi kuhakikisha wanalitunza vizuri jengo hilo ikiwa na pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na TAWA ndani ya hifadhi hiyo.

Katika hatua nyingine, Kamishna huyo ameupongeza uongozi wa Pori hilo  kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kulinda rasilimali walizopewa kusimamia kiasi cha kuwavutia wawekezaji.

"Nimefarijika sana wakati napokea taarifa yenu kujulishwa kwamba Pori la Akiba Moyowosi lina vitalu vya uwindaji wa kitalii 6 , na kati ya vitalu hivyo 6 vitano vina wawekezaji" amesema.

"Niseme tu kwamba hawa wawekezaji hawajaja bure wamekuja hapa kwasababu kuna rasilimali na hii rasilimali ipo kwasababu ya kazi yenu nzuri, mmefanya kazi nzuri ya kuhakikisha wanyama  walioko kule  porini na mazingira yao yako salama..kwahiyo niwapongeze sana kwa hilo" ameongeza.

Kwa upande wake Kamanda wa Pori la Akiba Moyowosi David Mnyapwani ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Menejimenti ya TAWA kwa jitihada za dhati za kuwezesha miradi inayotekelezwa katika Hifadhi hiyo kujengwa na  kukamilika kwa wakati

Ujenzi wa mradi huo ulianza kutekelezwa   Mei 05, 2023 na kukamilika Septemba 09, 2023 na tayari umeanza kutumika.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...