Skip to main content

MVUA ZA EL - NINO NI SABABU YA ONGEZEKO LA MAMBA KASAHUNGA NA MAYOLO - DC BUNDA


Na. Beatus Maganja 

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Dkt. Vicent Anney amesema mvua za El Nino zimekuwa sababu kubwa ya ongezeko la wanyamapori aina ya mamba ambao wamekuwa wakitoka maeneo yao ya asili na kwenda maeneo ya wananchi na kuleta madhara kwa maisha na mali zao katika vijiji vya Kasahunga na Mayolo Wilayani Bunda.

Dkt. Vicent ameyasema hayo leo Januari 18, 2024 katika ziara ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA, Mabula Misungwi Nyanda iliyofanyika wilayani humo kwa lengo la kuwatembelea waathirika wa mamba na kutoa pole.

"Na mwaka huu, Kamishna hali hii imeongezeka sana baada ya kuwepo kwa mvua ya El Nino ambayo imesababisha mamba kutoka katika maeneo yao ya asili kwenda kusogea kwenye maeneo ya wananchi" amesema.

Akifafanua zaidi suala hilo, Dkt. Vicent amesema  mamba  wamekuwa wakisafirishwa na mikondo ya maji ya mito  kuelekea ziwani jambo ambalo limesababisha wanyamapori hao kuonekana kwa wingi katika kingo za Ziwa Victoria nyakati za jioni na alfajiri na hivyo kusababisha madhara kwa baadhi ya wananchi wanaokwenda kuchota maji au kuoga kando ya Ziwa hilo.

Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo,  Mkuu huyo wa Wilaya amepongeza jitihada za dhati zinazofanywa na timu ya Maafisa na Askari wa TAWA Kanda ya Ziwa akithibitisha kuwa  wanafanya kazi usiku na mchana katika harakati za kuwadhibiti mamba hao na kutoa rai waongeze kasi ya kutoa elimu ya kujikinga na kuwadhibiti wanyamapori hao kwa wananchi wa maeneo yenye changamoto hiyo.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda amesema kutokana na kuongezeka kwa vilio vya wananchi vinavyotokana na matukio ya mamba katika vijiji vya Kasahunga na Mayolo Wilayani humo, imemlazimu kufanya ziara mahsusi katika vijiji hivyo ili kujionea hali halisi ikiwa ni pamoja na kuwatembelea na kuwapa pole familia za ndugu walioathiriwa na wanyamapori hao na kufikisha salamu za rambirambi kutoka  Serikalini.

Kamishna Mabula amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii inayoongozwa na Waziri Angellah Kairuki wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya changamoto ya mamba inayowakabili wananchi hao na kuahidi kuongeza ulinzi  kwakuwa kipaumbele cha kwanza kwa Serikali ni uhai wa wananchi wake na siyo wanyamapori.

Kwa minajiri hiyo, Kamishna Mabula ametoa maelekezo kwa Maafisa na Askari wa TAWA kwa kushirikiana na wananchi kuwasaka mamba wote walioleta madhara kwa wananchi au wenye viashiria vya kuhatarisha maisha ya binadamu katika maeneo hayo na kuwaua kwa mujibu wa Sheria.

Pia amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuchukua tahadhari wanapofanya kazi zao pembezoni mwa Ziwa hilo ikiwa ni pamoja na kuweka makazi yao umbali wa Mita 60 kutoka ziwani.

Naye Diwani wa Kata ya Kasahunga Mhe.Fortunatus Maiga ameipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Kata hizo na hivyo ameiomba kujenga miundombinu ya maji katika Kata yake ili kuokoa maisha ya wananchi wanaokwenda kuchota maji ziwani pamoja na kuwavuna mamba hao ambao wanahatarisha maisha ya binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...