Skip to main content

KUELEKEA MASIKA 2024: TMA YAPONGEZWA KWA USHIRIKIANO NA WADAU

 

Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ameipongeza TMA kwa kuendelea kushirikisha sekta mbalimbali nchini katika shughuli za utoaji wa huduma za hali ya hewa. Alibainisha hayo wakati akifungua rasmi Mmkutano wa 24 wa Wwadau wa Uutabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2024 uliofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Dodoma, Tarehe 19/2/2024.

“Tunapoelekea kutoa utabiri wa mvua za Masika 2024, lengo kuu la kukutana hapa ni kuwezesha matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa wote na kwa wakati, ninapenda kuipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika shughuli zao za utoaji wa huduma za hali ya hewa ambazo ni pamoja na utabiri wa misimu ya mvua. 

Ushirikiano huu ni mfano wa kuigwa na unafaa kuendelea hasa katika kipindi hiki ambapo dunia pamoja na nchi yetu inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa”. Alisema Mh.Jaji Bakari

“Tunapojiandaa kupokea taarifa ya utabiri wa Masika, Machi hadi Mei, 2024 ni muhimu sana kila mmoja wetu kuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu, kuelewa, kupanga na kukabiliana na hali ya hewa inayotarajiwa katika sekta yake”. Alisisitiza Jaji Mshibe Bakari.


Awali, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri TMA, Dkt. Hamza Kabelwa alisema “Mkutano huu ni mwuendelezo wa sehemu ya ushirikishwaji wadau hususan wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika kuandaa taarifa zinazolenga kuchochea matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa. 



Katika mkutano huu tutakuwa na majadiliano ambayo ni muhimu katika kuendeleza na kuimarisha utoaji wa huduma za hali ya hewa na matumizi yake kwa jamii. Mkutano huu ni muhimu sana kwa wadau wa hali ya hewa katika kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zao”.  


Naye mwakilishi kutoka Sshirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme - WFP) Sasha Guyetsky, Mkuu wa Utafiti, Tathmini na Ufuatiliaji, WFP Tanzania,  aliishukuru TMA kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa WFP pamoja na wadau wengine nchini., Aaidha, alieleza kuwa hivi karibuni TMA na WFP wamesaini ushirikiano wa miaka mitano wa kiutendaji ili kuweza kuimarisha utoaji huduma za hali ya hewa wenye kuleta tija.

Mmoja wa wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mbanga alieleza namna taarifa za awali za msimu wa mvua za Vuli, 2023 zilivyosaidia katika kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo pamoja na kuandaa Mmpango Taifa wa Ddharura kwa mikoa iliyotarajiwa kuathirika kutokana na hali ya El NiƱo.


Katika mkutano huu, wadau walipata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei, 2024 na kutoa michango yao juu ya athari zinazotarajiwa katika sekta husika pamoja na ushauri ili kuwezesha kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...