Skip to main content

MKUU WA MKOA WA LINDI AWATAKA WAKAZI WA KILWA KUWA TAYARI KUWAPOKEA WATALII


Na. Beatus Maganja

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab Telack amewataka wakazi wa wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla kuwa tayari kuwapokea watalii wanaotembelea Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara na kutumia fursa hiyo kufanya biashara za bidhaa za utalii ili kuwaingizia kipato.

Mhe. Zainab ameyasema hayo Februari 28, 2024 akiongea na waandishi wa habari ndani ya Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara wakati wa mapokezi ya Meli ya Saba kuingia Hifadhini humo katika kipindi cha mwezi Februari ikiwa na idadi ya watalii 120 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani.

Amesema mfululizo wa safari za Meli za watalii ndani ya Hifadhi hiyo ni kiashiria kwamba filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyochezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta matokeo chanya kwa Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara iliyo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA inatarajia kupokea Meli nyingine zaidi za watalii Mwezi Machi na April hivyo wakazi wa Mkoa huo watumie vyema ujio wa Meli hizo.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwaalika watu wote wenye bidhaa zinazopendwa na watalii na kuziuza wakati wa safari za wageni ndani ya Hifadhi hiyo huku  akisisitiza kuwa TAWA imejenga jengo la kisasa na maalumu kwa ajili ya wafanyabiasha wa bidhaa za kitalii, hivyo walitumie jengo hilo ipasavyo.

Akibainisha sababu za watalii wengi kutembelea Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mkuu wa Hifadhi hiyo Mercy Mbogelah amesema majengo ya kale yaliyojengwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita kama vile msikiti mkubwa na mkongwe kuliko yote katika ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki na ngome ya Mreno ni vivutio vikubwa vya watalii vinavyowafanya watalii wengi kumiminika katika Hifadhi hiyo 

Amesema kutokana na historia hiyo kubwa ndani ya Hifadhi ya Kilwa kisiwani  Mwaka 1981 Shirika la Kimataifa la UNESCO liliipa hadhi Hifadhi hiyo na kuwa Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa Dunia na baadae Mwaka 2023  kuwepa hadhi nyingine kuwa "Man and Biosphere Reserve". Vigezo vyote hivi vimetajwa kuwa mojawapo ya sababu za watalii wengi kutoka nje kupenda kuitembelea.

Maboresho  ya miundombinu wezeshi ya utalii yaliyofanywa na Serikali kupitia TAWA nayo imetajwa kuwa miongoni mwa sababu za watalii wengi wa ndani na nje kupenda kutembelea na Kutalii ndani ya Hifadhi hiyo.

Naye Afisa Utalii wa Hifadhi hiyo, Shindawangoni Rajabu amesema Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara imekuwa ikipokea Meli kubwa za watalii na Mwaka huu wa 2024 imepokea Meli nyingi zikiwa na idadi kubwa ya watalii katika kipindi kifupi ikilinganishwa na miaka mingine yote na inatarajia kuendelea kupokea Meli nyingine zaidi za watalii kutoka Mataifa mbalimbali Duniani.

Amesema ongezeko la idadi ya Meli zenye idadi kubwa ya watalii ni kiashiria tosha kuwa Hifadhi hiyo inaendelea kivutio kizuri zaidi Duniani.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...