Skip to main content

ONGEZEKO LA MVUA MWEZI MACHI , TMA YATOA TAHADHARI



Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa mvua za masika kwa msimu wa mwezi Machi hadi Mei kwa mwaka 2024 ambapo mvua zinatarajiwa kuwa wastanibhadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Lasdaus Chang'a amesema kuwa mvua za masika zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi febuari 2024 katika maeneo mengi, huku ongezeko la mvua likitarajiwa katika kipindi cha mwezi Machi 2024.

"katika maeneo mengi mvua  zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2024 katika maeneo mengi, huku miongoni mwa athari zinazotarajiwa kutokea ni pamoja na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafuzi wa maji, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka na vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo"amesema Dkt Chang'a.

Aidha amesema mvua za Masika ni mahsusi kwa maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki ( mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), Pwani ya Kaskazini ( Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani ikijunuisha visiwa vya Mafia, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba), ukanda wa ziwa Victoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Hata hivyo, amesema mifumo ya hali ya hewa joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya Hindi (Pwani ya Afrika Mashariki) ikilinganishwa na upande wa Mashariki mwa bahari ya Hindi huku joto la bahari la chini kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo ya kusini mwa kisiwa Cha Madagaska.

Sambamba na hayo amesema kutoka na hali hiyo wakulima wameshauriwa kuandaa mashamba, kupanda na kupalilia na kutumia pembejeo husika Kwa wakati, kutumia mbinu bora na teknolojia za kuzuia Maji kutuama shambani, mmomonyoko na upotevu wa rutuba na kuchagua mbegu na mazao sahihi Kwa ajili ya msimu huu wa Masika.

Hata hivyo ametoa wito kwa Menejimenti za maafa kuwa vipindi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na kupelekea uharibifu wa miundombinu, mazingira, upotevu wa mali na maisha hivyo mamlaka husika ziendelee kuratibu utekelezaji wa mipango ya kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...