Skip to main content

RELAXO MPYA YAZINDULIWA DAR, SERIKALI YAWAHAKIKISHIA USALAMA WAWEKEZAJI

  


Na Mwandishi wetu, HabariPlus, Dar

Kampuni Best Brand Distributor leo wamefungua duka jipya la tatu la viatu vya Relaxo aina zote 'show room' mtaa wa Morogoro /Samora ambapo ya kwanza lipo Mlimani Cty na la pili Mtaa wa Nkurumah eneo la kati kati ya jiji Clock Tower.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Best Brand Distributor Khalid Salim amesema kuwa lengo la Kampuni hiyo ni kufungua maduka mengine 20 ifikapo 2025 huku akiahidi kuwa kama soko la bidhaa hizo litakua rafiki wanatarajia kufungua kiwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizo nchini Tanzania.

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuwezesha kuwa na mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana zaidi ya nchi ya Tanzania.

Awali akikata utepe katika duka hilo kama ishara ya uzinduzi wa show room hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema Serikali inawahakikishia kuboresha mazingira ya usalama kwa wawekezaji na kuendelea kuwapa ushirikiano ili kusaidia Serikali kutoa ajira za kudumu za muda mfupi kwa wazawa.

Amesema kuwa, Serikali peke yake haiwezi kutoa ajira kwa vijana wote nchini hivyo panapotokea wawekezaji wengi inaleta faraja na mtazamo mzuri kuhakikisha vijana wanaendelea kutafuta vipato vyao kupitia wawekezaji wenye dhamira ya dhati kumsaidia Rais Dkt Samia katika kuhakikisha wanapata fursa nyingi za ajira na viwanda.

"Nitoe pongezi sana kwenu kwa kuisaidia Serikali, kama mnataka kuanzisha kiwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizi niwahakikishie tupo pamoja na nyinyi Serikali imetenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji, mutasaidia kwenye mzunguko wa fedha "amesema Kumbilamoto.

Akizungumza katika hafla hiyo Mpoki amesema kuwa show room hizo 20 zitakazofunguliwa lengo ni kuwarahisishia wateja wao kupata huduma zao pembe zote za jiji la Dar es Salaam na zikifuatiwa na show room 2 au 3 kwa mikoa yote ya bara na visiwani.

Salim kikeke ni miongoni mwa wanafamilia wa Relaxo waliofika katika uzinduzi huo  amesema kuwa show room hizo ni mahsusi kwa brand maaruf za viatu Sparx, Flite Telaxo na Bahamas zinazosheheni viatu vya aina mbalimbali vya kutembelea na matumizi mengine.

"Katika show room hizi zina viatu mbalimbali ikiwemo viatu vya mazoezi vya kike na kiume, shule, maabara, hospital madokta na manesi yaani tumesheheni viatu aina zote vya wakati wote kwa mazingira yote ambavyo tunauza jumla na reja reja"amesema Kikeke



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...