Skip to main content

TAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA UTALII KILWA - DC KILWA


Na. Beatus Maganja

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Emil Ngubiagal amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ni taasisi iliyoleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Utalii na kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali na wazawa wa wilaya hiyo kutokana na maboresho ya miundombinu ya utalii katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara yanayopelekea watalii wengi kutembelea Hifadhi hiyo.

Komredi Ngubiagal ameyasema hayo Februari 25, 2024 akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo ikiwa ni siku moja baada ya meli iliyobeba watalii 146 kutia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara.

"Naipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya sita kwa kuona sasa utalii katika wilaya ya Kilwa ni vyema tupeleke taasisi inayoitwa TAWA ili kusudi ikasimamie, ikaendeleze, ikaboreshe hii Sekta nzima ya utalii ya wilaya ya Kilwa" amesema Mhe. Christopher Ngubiagal

"Kwakweli kwasasa hivi unavyoona maendeleo makubwa katika Sekta hii ya utalii Kilwa yameletwa na Taasisi ya TAWA, Leo ukifika Kilwa kisiwani utaona mabadiliko makubwa katika miundombinu" ameongeza Mkuu huyo wa wilaya.

Mhe. Christopher amesema awali kabla ya ujio wa TAWA wakazi wa wilaya yake pamoja na watalii walikuwa wakipata adha ya kufika Kilwa kisiwani kutokana na uduni wa miundombinu lakini baada ya kuingia TAWA walipeleka boti za Kisasa ambazo zinawafanya watalii na wazawa hao kufika hifadhini kwa raha mstarehe.

Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza soko la utalii aliposhiriki filamu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imeleta mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea.

Naye Said Amri Said mkazi wa Kilwa kisiwani amekiri kuwa ujio wa TAWA katika Hifadhi hiyo umechangia  kuongeza idadi ya watalii ambapo kupitia wageni hao wakazi wa eneo hilo wananufaika kiuchumi kwa kufanya biashara ndogo ndogo ambazo zinawaingizia kipato.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya hiyo kutumia fursa ya ujio wa Meli za watalii kujiongezea kipato kwa kuuza bidhaa pendwa kwa wageni kama vile vitu mbalimbali vya asili na  kiutamaduni.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...