Skip to main content

TMA YAWANOA WANAHABARI KUELEKEA MASIKA 2024

 

Dar es Salaam; Tarehe 21, Februari 2024

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali kujadili kuhusu utabiri wa msimu wa Masika (Machi –Mei) 2024, unaotarajiwa kutolewa tarehe 22 Februari 2024. 

Utabiri huo ni mahususi kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro, Visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga, Kilimanjaro,Arusha, Manyara,Simiyu, Mara, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kagera na Kaskazini mwa Kigoma. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE), Dar es Salaam, Tarehe 21/2/2024.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi, Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, alisema “Mkutano huu ni mwendelezo wa sehemu ya ushirikishwaji wa wanahabari katika kuandaa taarifa zinazolenga kuchochea matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa”. 

Aidha aliendelea kusisitiza kuwa, uzingatiaji wa taarifa  za hali ya hewa, hususan tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya watu na mali zao na katika kuongeza tija na ufanisikatika kupanga na kutekeleza mipango ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo katika sekta za kilimo, ujenzi, Afya, Maji, Ulinzi, Usafiri (Anga, Maji na Nchi Kavu), Madini, Utalii, shughuli za Bandari nk..

Dkt. Chang’a alisema kwa kuzingatia umuhimu huo wa huduma za hali ya hewa nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi chake imeendelea na jitihada za kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini ikiwemo uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu ya uangazi, uchakati wa data na utabiri, ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Ibara ya 59J.

Hivyo, aliishukuru Serikali na wadau wa maendeleo kwa kuendelea na uwekezaji katika miundombinu ya hali ya hewa hapa nchini kupitia mpango wa bajeti na programu mbalimbali za maendeleo, hali inayochangia Mamlaka kuendelea kuboresha huduma zake. 

Naye Mwakilishi wa washiriki kutoka gazeti la Majira, Bi. Penina Malundo,  aliishukuru TMA kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa waandishi wa habari  katika kuhakikisha wanaandika habari za hali ya hewa kwa ufanisi na uweledi ili wananchi waweze kuelewa. 

“Utoaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari umeweza kuongeza tija kwa wananchi kufuatilia taarifa hizo katika kufanya shughuli zao hususan za kijamii”. Alisema Bi. Penina.

Katika mkutano huu, wanahabari walipata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei, 2024 na kutoa michango yao juu ya namna sahihi ya usambazaji wa taarifa katika kipindi chote cha msimu.



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...