Skip to main content

WALIOFUNGA VING'ORA, NAMBA BANDIA, VIMULIMULI KWENYE MAGARI NA PIKIPIKI KIAMA CHAO CHAJA

Na Mwandiahi wetu, Habari Plus, Dar

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kimepiga marufuku wamiliki na madereva wote nchini kutoweka Ving'ora, Vimulimuli, Namba bandia na taa za kuongezwa kwenye magari na pikipiki kama kuna ulazima wa kufanya hivyo basi wanatakiwa kuomba ridhaa ya kupata kibali cha kufanya hivyo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Aidha, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kitaanza oparesheni kabambe ya kukamata magari yote na pikipiki ambayo si ya dharura na yamefungwa ving'ora bila kuzingatia utaratibu wa kisheria kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukulia dhidi yao ikiwemo kupelekwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Ramadhan Ng'anzi amesema kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtu yoyote kufunga king'ora katika gari au pikipiki bila kuzingatia utaratibu wa kisheria na kanuni za usalama barabarani zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

"Wapo baadhi ya wananchi ambao wamegeuza ving'ora kuwa fasheni  katika magari au pikipiki zao, tukumbuke kuweka king'ora cha aina yoyote katika gari au pikipiki ni lazima ufuate sheria tutawakamata kuanzia leo wote watakaokaidi agizo hili na tutawachukulia hatua"amesema Kamanda Ng'anzi.

Aidha, amesema kuwa,kuna baadhi ya watu, makampuni na taasisi mbalimbali zimekuwa zikivunja sheria ya usalama barabarani, na  wanastahi adhabu ikiwemo ya kulipa faini ya tozo za makosa ya usalama barabarani au kuwekwa mahabusu na kuandaliwa mashtaka na kupelekwa mahakamani au vyote kwa pamoja.

Aidha, amesema kuwa ni kosa kisheria kufunga taa zenye mwanga mkali zinazoongezwa kwenye magari au pikipiki yaani spot light na led bar wanafunga kama urembo kwenye magari na pikipiki na wanatakiwa wavitoe mara moja kwani wamefunga kwa kinyume cha sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani.

"Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani litafanya oparesheni kali kudhibiti ufungwaji wa taa zinazoongezwa kwenye magari na pikipiki, kuna watu wanaweka Taa za kuongezwa kwenye magari, nyuma ya magari makubwa hususani malori, wananchi wenye tabia hii waache mara moja kwani ni kinyume cha sheria"amesema Kamanda Ng'anzi.

Ameongeza pia ni kosa kisheria gari au pikipiki kubandikwa namba bandia zisizo na usajili, ambapo baadhi ya watu wamejenga utamaduni ambao wanajihalalishia kuwa ni sheria kuweka namba bandia kwenye magari, hivyo wanatakiwa watoe mara moja namba hizo kabla ya oparesheni kuanza.

Sambamba na hayo, amesema kunavmagari ambayo yamewekwa taa kutoka kiwandani hizo zinaruhusiwa kisheria mfano magari ya mgodini tu na kwenye mapori wakati wa uwindaji na sivyenginevyo, hivyo anapotoka maeneo hayo aweke kava za kuzuia mwanga mkali barabarani kwani mwanga huo unaweza kusababisha uoni hafifu.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...