Skip to main content

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YARIDHISHWA NA MABORESHO KIWANDA CHA KUTENGENEZA MASHINE NA VIPURI CHA KMTC-MOSHI

 

Na Mwandishi Wetu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo, Mifugo na Uvuvi imelipongeza shirika la Taifa la Maendeleo( NDC) kwa kuboresha Kiwanda cha KMTC na kuendelea na uzalishaji wa Vipuri pamoja na Mashine mbalimbali kama ilivyokusudiwa wakati wa uanzishaji wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia kitengo Cha Mawasiliano na Masoko NDC,Machi 13 ,2024 ,pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Mjini Deo Mwanyika mara baada ya kamati hiyo ya kudumu ya bunge kutembelea kiwandani hapo na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika kiwanda hicho kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Aidha Mwanyika amesema kuwa KMTC ni kiwanda kikubwa cha kuzalisha viwanda vingine na kina mchango mkubwa kwenye uchumi huku akibainisha kuwa malighafi kubwa ya kiwanda hicho ni chuma kinachotumika kutengeneza vipuri na mashine na kama Taifa tukitaka kufikia malengo lazima tuanze Uchimbaji wa chuma cha Liganga.

"Nimshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa kiwanda hiki kwenye matumizi ya chuma, hivyo kuamua kutoa fedha za fidia kule Liganga ili chuma kile kitumike kiwandani hapa," amesema Mwanyika.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji ameeleza kuwa wao kama Wizara yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya viwanda hapa nchini wanafurahi kuona kazi ya kuyeyusha chuma imeanza kiwandani hapo hivyo kurejesha ajira kwa Watanzania ambao walikosa ajira kwa muda mrefu, huku akiishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizofanikisha ujenzi wa tanuru la kuyeyusha chuma (foundry) Pamoja na mtambo wa kutia utandu kwenye chuma (Galvanising plant).

"Ninamshukuru sana Mh. Rais wetu kwa maono yake na kuyatekeleza maono hayo na amewathibitishia Watanzania kuwa Taifa letu litajengwa kwa Uchumi wa viwanda hasa viwanda mama kama KMTC," amesema Dkt. Kijaji.

Hata hivyo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amir Mkalipa amewakaribisha wafanyabiashara mbalimbali kununua bidhaa zinazozalishwa na KMTC pia amewataka wenye viwanda kutohangaika kutafuta vipuri vya mitambo yao na kulazimika wakati mwingine kuagiza nje ya nchi kwani KMTC wana uwezo wa kuchonga vipuri hivyo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe ameeleza kuwa bidhaa zinazozalishwa na KMTC zinagusa sekta mbalimbali kama kilimo, viwanda, uchukuzi, usafirishaji, madini, misitu na ujenzi hivyo kuwa ni kiwanda chenye manufaa katika sekta hizo.

 Licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada inazozifanya katika kukiendeleza kiwanda hicho Dkt. Shombe amebainisha kuwa Serikali imeendelea kufanya juhudi mbalimbali ili kuhakikisha kiwanda hiki kinaboreshwa na hatimaye kiweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda nchini na kuinua maisha ya wananchi na kutoa ajira ambapo mpaka hivi sasa ujenzi wa tanuru la kuyeyusha chuma pamoja na mtambo wa kutia utandu kwenye chuma umeshakamilika.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...