Skip to main content

PURA NA DMI KUSHIRIKIANA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI BAHARINI

 

Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petrol (PURA) wamewekeana hati ya Saini ya ushirikiano na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) katika kupata wataalamu wakufunzi watakaosaidia usalama katika shughuli za uchimbaji Mafuta na gesi baharini kupitia Mradi wa NLG.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi jijini Dar es Salaam Mtendaji PURA, Charles Sangweni amebainisha kuwa hadi kufikia Februari 2024 idadi ya mikataba iliyosainiwa imefikia 11 ambapo kati ya mikataba hiyo 8 ipo katika hatua za utafutaji na 3 ipo katika hatua za uzalishaji.

"Hatua za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini zilipelekea kufanyika kwa ugunduzi wa gesi asilia kwa mara ya kwanza katika kitalu cha Songosongo mwaka 1974 na kitalu cha Mnazibey1982 ambapo gunduzi hizo ilifanyika katika maeneo ya nchi kavu na maeneo ya kina kifupi cha bahari pia ugunduzi mwingine umefanyika katika maeneo ikiwemo Mkuranga,Mtwara,Ruvu na katika maeneo ya kina kirefu cha Bahari Hindi Kusini mwa Tanzania" amesema.

Aidha, amesema hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu jumla ya futi za ujazo Tilion 57.54 zote ni za gesi asilia kati ya kiasi hiko futi za ujazo tilioni 10.406 ziligundulika nchi kavu na kina kifupi cha bahari huku futi za ujazo zilizobaki Tilion 47.13 ziligundulika maeneo ya kina kirefu cha bahari.

Hata hivyo amesema kwa kiasi gesi asilia ambacho kipo nchi kavu tilion 10.406 ambapo mpaka sasa gesi iliyotumika ni kiasi cha Tilion 0.7 ni kutoka Songosongo hivyo ifahamike kuwa ni kiasi kikubwa bado hakijachimbwa na Serikali iliamua kuuza gesi nje ya nchi kupitia Mradi wa NLG na kwa sasa wapo katika Mazungumzo na wagunduzi.

"Mradi wa NLG utakapoanza utekelezaji wake tunatarajia kuchimba visima ziada zaidi ya 30 na vitachimbwa ndani ya Bahari kuu kilomita zaidi ya 100 kwenda baharini kutoka ufukweni kilomita zaidi ya 3 kwenye sakafu ya maji kwenda chini kilomita mpaka 2 hivyo zitakuja Meli kubwa zenye uwezo mkubwa wa kuchimba visima kwa wakati mmoja na Meli zote zinahitaji huduma ikiwemo vyakula na huduma nyinginezo "amesema Sangweni.

Sambamba na Mkurugenzi amewasisitiza Wananchi ni wakati muafaka wa wachangamkie fursa zilizopo na hasa kwa anayetamani kufanya kazi katika maeneo lazima awe na kibali ambacho kinaonyesha kuwa amepata kozi fupi katika chuo cha bandari(DMI) za Usalama kwani anapoenda kufanya kazi inahitajika Usalama wa mali anayoisimamia na yeye mwenyewe.

Hata hivyo, amesema PURA na DMI walikaa na kuona ni gharama kuagiza wataalamu kutoka nje hivyo ni bora watumie wataalam kutoka katika chuo hiko na anayehitaji akapate mafunzo kabla ya mradi kuanza kwani ni elimu ni akiba.

Aidha shughuli hizo za upatikanaji wa Mafuta na gesi asilia zinatekelezwa kwa kufuata sheria ya Petroli ya mwaka 2015 ambapo hutekelezwa kwa huangalia mikataba iliyo katika makubaliano ya ugawanyaji wa Mapato iliyoingiwa na serikali, ShirikaTPDC .

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) Dkt Tumaini Gurumo amesema uchimbaji wa Mafuta na gesi baharini ni eneo ambalo linahitaji usalama kwanza ufanyike ufundi wote lakini suala la usalama lazima liwe mwanzoni ndiyo maana kabla ya kuingia katika chombo chochote majini ikiwemo Meli yeyote mwanzoni hutolewa namna ya kujiokoa pale janga linapotokea na namna kuokoa wengine ikihusisha huduma ya kwanza.

"Shughuli za uchimbaji Mafuta na gesi hufanyika baharini na hakuna hospitali hivyo mafunzo ni muhimu ya usalama Chuo cha DMI kina ithibati ya Kimataifa kutoa mafunzo ya elimu kwa Mabaharia wengi wameajiriwa katika meli mbalimbali nje na ndani ya nchi"amesisitiza Dkt Tumaini



Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...