Skip to main content

TBPL NA KAMPUNI YA JJ YASAIN MKATABA WA USAMBAZAJI VIUATILIFU

 

Na Mwandishi wetu

Serikali kupitia kiwanda cha Biotech Product Limited (TBPL) kilichopo Kibaha Pwani kimetiliana saini imkataba wa miaka 3 na kampuni ya JJ Agricultural ltd ya kusambaza  dawa mpya viuatilifu hai ambazo zitatumika kupambana na wadudu dhurifu wa mazao mbalimbali ya kilimo.

Aidha, miongoni mwa mazao hayo ni pamoja na Pamba, Mahindi, Matunda  na Mbogamboga hali itakayosaidia kupatikana kwa dawa hizo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba huo Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Rafael Rodriquez ameonyeshwa kufurahishwa na makubaliano waliyofikia na kampuni ya JJ Agricultural Limited ambapo amebainisha kuwa hatua hiyo ni mafanikio makubwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata fursa ya kufikiwa na bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

"Tunatambua changamoto inayowakabili wakulima ya uwepo wa wadudu dhurifu katika mazao yao makabaliano haya yanakwenda kuwasaidia wakulima katika kupatikana kwa dawa hii hali itakayowafanya wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika mazao yao" amesema Rodriquez.

Aidha, ametumia fursa hiyo kubainisha sifa za kipekee za dawa hizo za viuatilifu kuwa ni tofauti na dawa zingine zinazopatikana sokoni kwa kuwa zenyewe zimetengenezwa kwa namna ya viuatilifu hai ikilinganishwa na dawa zingine zisizo za kibaolojia kwa kuwa zinapelekea madhara watumiaji kama vile magonjwa ya kansa pamoja na kuharibu mazingira huku akiwataka mawakala zaidi kuendelea kujitokeza kwa wingi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya JJ Agricultural Ltd, Mhandisi James Kilaba ameishukuru TBPL kwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba huo huku akiomba kupewa ushirikiano katika kipindi chote cha utekelezaji wake ambapo miongoni mwa kazi zitakazofanywa na kampuni hiyo ni pamoja na kuhakikisha wanaandaa mashamba darasa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambayo yatatumika katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya namna bora ya kutumia dawa hizo katika kupambana na wadudu dhurifu katika mazao yao.

Sambamba na hayo mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitatu ambapo kwa kuanzia dawa hizo zinatarajia kupatikana katika mikoa ya Dar es salaam Pwani, Morogoro, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Iringa, Dodoma Singida, Katavi pamoja na Tanga na utahusisha pia utoaji wa mafunzo ya namna bora ya kutumia dawa hizi ambao utakuwa unafanywa na wataalam kutoka katika kiwanda cha TBPL.

Kiwanda cha Kibaolojia cha TBPL ni kiwanda pekee kilichopo nchini na barani Afrika ambacho kinamilikiwa na serikali na kinazalisha dawa za kibaolojia hapa nchini ambapo kinazalisha dawa za Viuadudu vya kupambana na Maleria (biolarvicides) ambapo kwa sasa mara baada ya kubaini uwepo wa changamoto za wadudu dhurifu katika kilimo imeanza rasmi uzalishaji wa dawa za viuatilifu hai vya kilimo (biopesticides) ambavyo ni bora na rafiki wa mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...