Skip to main content

TEHAMA KUFADHILI WANAWAKE 100 KONGAMANO LA USALAMA MTANDAO

 

Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar

Tume ya Habari na Mawasiliano nchini (TEHAMA), imeendaa jukwaa la tatu la usalama wa mitandao ya kielekitroniki la mwaka 2024 litakalofanyika kuanzia April 4 hadi 5 mwaka huu jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine litawafadhili kwenda kwenye kongano hilo wanawake 100 ambao wanaujuzi kuhusiana na masuala ya Tehama.

Akizungumza na wanahabari  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Tume hiyo, Dkt Nkundwe  Mwasaga amesema kongamano hilo litashirikisha jumla ya washiriki na wadau mbalimbali zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo ajenda kuu tano andani ya mkutano huo zitajadiliwa ikiwemo mkakati wa uchumibwa kiditali na huduma za mawasiliano kuwa jumuishi.

Nkundwe amesema wao kama nchi wenyeji wameamua kutoa ufadhili kwa washiriki wanawake 100 watakaolipiwa gharama zote za ushiriki wa kongamano hilo ili kuwapa motisha kushiriki kwenye masuala ya usalama wa kimtandao kwani lengo la Tume hiyo ni kuhakikisha kila mtu anakuwa na uwelewa kuhusu usalama wa mtandao.

Aidha amewataja baadhi ya wadau watakaoshiriki kongamano hilo kuwa ni pamoja na wale wanaojishughulisha na kutengeneza tafiti, kuelimisha na kusimamia, kuandaa miongozo mbalimbali ya matumizi Salama ya mitandao ya kompyuta na matumizi ya kielekroniki kwa hapa nchini.

Katika hatuna nyingine amesema sababu za kuandaa kongamano hilo hi ni kuangalia zaidi masuala ya kimtandao ikiwemo matumizi ya fedha na haki za mtu binafsi pia kuzuia mashambulizi ya maswala ya kielekroniki na mitandao ya nchi kiusalama.

Ameongeza kuwa ajenda nyengine ni pamoja na  kuratibu sera ya tehama pamoja  kufanya mageuzi ya kidigitali na kuwapa ujuzi watanzania kuhusu maswala ya tehama.

Aidha pia madhumuni mengine ya mkutano huo ni pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano ambayo ni jumuishi kwa makundi yote bila kubagua jinsia pamoja na kuzuia ushawishi wa makosa ya kimtandao ambayo yanafanywa na watu bila kujua kuwa kufanya hivyo ni makosa kisheria.

Amesema kwa mujibu wa takwimu za kidunia Tanzania Inashika nafasi ya pili kwa usalama wa kimtandao huku nchi ya Mauritius ikiwa ndio kinara kwenye usalama wa maswala ya makosa ya kimtandao na kielekroniki duniani.

Aidha ametoa wito kwa wananchi na wadau wengine kujitokeza kushiriki kongamano hilo kwani linamanufaa kiuchumi na kijamiii kwa mtu Mmoja Mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema kutokana na sifa ya kuwa nchi ya pili kiusalama kimtandao wawekezaji wengi kutoka mataifa mbali mbali yameonyesha Nia ya kuja kuwekeza nchini huku akitoa tahadhari kuwa nchi yoyote isiyokuwa na usalama wa mitandao wawekezaji hawawezi kuwekeza mitaji kwa sababu za kiusalama.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo ametaja gharama na ada ya ushiriki wa kongamano la mwaka 2024 kuwa ni shilingi 250,000 kwa wataalamu wa tehama waliosajiliwa na tume ya hiyo na wale wasiosajiliwa watalipia shilingi 300,000 kwa ushiriki wao.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...