Skip to main content

ZARI AONGEZA MKATABA DOWEI CARE TECHNOLOGY

 

Na Mwandisi wetu, Habari Plus 

Kampuni ya Dowei Care Technology ambao ni wazalishaji wa Taulo za kike na za watoto (SOFTCARE) kesho wanatarajia kutoa msaada wa bidhaa zao katika hospital ya Taifa ya Muhimbuli katika kitengo cha huduma za mama mtoto lengo likiwa kuendelea kumsaidia mwanamke kujisitiri pindi anapokuwa kwenye siku zake za hedhi.

Akizungumza leo Machi 21,2024 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari wakati wakisaini mkataba mpya na balozi wa bidhaa hizo ambae ni mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan (Zari the boss lady),  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Victor Zhang amesema wamekuwa wakipata matokeo chanya na yenye tija kutokana na uwepo wa boalozi huyu.

Amesema kuwa, kampuni yao wamekuwa wakirudisha faida kwa jamii kwa kushiriki kampeni nyingi za kitaifa ikiwa ni pamoja na ugawaji wa taluo za kike kwa mabint wa shule za msingi na Sekondari.

"Tumekuwa tukipata matokeo chanya kwa kumtumia huyu balozi wetu lakini pia kutokana na mtokeo hayo tumekuwa na utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii tunawapunguzia mzingo mabint kwa kukosa taulo za hizo jambo ambalo linawasababishia kukosa masoma pindi wanapokuwa kwenye hedhi zao"amesema Zhang.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo kufanya kazi na balozi huyo amesema wameamua kuendelea na kufanyakazi na Zari kwa maana ameweza kuleta matokeo chanya kwa kampuni yao kwani wamezidi kupata faida.

Kwa upande wake, Zarina Hassan ambae ni balozi ya bidhaa hizo amesema kampuni hiyo ina kila sababu ya kumuongezea mkataba kwani kupitia yeue kampuni hiyo imekua ikifanga vizuri kwenye soko kutokana na umaarufu wake.

Aidha, ameishukuru kampuni hiyo ya Dowei kwa kumpa mkataba mwingine tena mnonno huku akiahidi kuendelea kuwasaidia wanawake na watoto wanaoshindwa kupata huduma ya taulo hizo kutokana na kuwepo kwenye mazingara magumu.

"Nitahakikisha bidhaa hizi zinafika kwa watu maskini na wenye uhitaji hususani wanawake na watoto wa kike ambao wanaishi kwenye mazingira magumu"amesema Zarina.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...