Skip to main content

TAWA YAPOKEA MELI YA WATALII ZAIDI YA 200 KILWA KISIWANI


Na Beatus Maganja 

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA leo Aprili 24, 2024 imepokea meli  ya watalii wapatao 230 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani  waliofika katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara kwa ajili ya shughuli za utalii.

Meli ijulikanayo kwa jina la "Silver Clouds" ndiyo iliyotia nanga katika Hifadhi hiyo ikiwa imebeba watalii kutoka Mataifa ya Australia, Ubeligiji, Brazil, Canada, Chile, China, Ujerumani, Ireland na Norway huku watalii wengine wakitokea Mataifa ya Italia, Ureno, Africa ya Kusini, Hispania, Sweden, Switzerland, Ukraine, Uingereza na Marekani.

Huu ni mwendelezo wa safari za watalii kutoka kona mbalimbali za Dunia kuja kujionea fahari ya urithi wa Dunia wa utamaduni, historia na malikale uliopo katika Hifadhi hiyo inayosimamiwa na TAWA.

Ikumbukwe kuwa Hifadhi hii imekuwa ikipata wageni wengi wa ndani na nje ya nchi yetu ambapo hivi karibuni (Februari, 2024) Hifadhi hiyo ilipokea zaidi ya watalii wa nje 900 kutoka sehemu mbalimbali  Duniani kwa ajili ya shughuli za utalii, idadi inayotajwa kuvunjarekodi katika Hifadhi hiyo.

Watalii hao wakiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Takim Holidays walipokelewa na kukaribishwa kwa ngoma za asili ya watu wa Kilwa Kisiwani iitwayo kitupolo ambayo iliwafanya waonekane kuwa na bashasha muda wote 

Tanzania  inaendelea kunufaika na kazi kubwa iliyofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipocheza filamu maarufu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imefungua milango kwa watalii wengi kuingia nchini kwa ajili ya shughuli za utalii.




Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...