Skip to main content

TANZANIA MWENYEJI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA


Na Mwansdishi wetu,HabariPlus

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya miaka 20 ya baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika yatakayofanyika Mei 25, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema kuwa ni heshima kubwa Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ambapo wageni 120 wanatarajiwa kuhudhuria kutoka nchi mbalimbali.

Amesema kuwa, Tanzania kuongoza maadhimisho hayo ni heshima kubwa kwani ni nchi 15 tu kati ya nchi 55 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Afrika, ndio wajumbe wanaounda baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika.

"Nchi ambazo zina wajumbe wa baraza hilo ni Tanzania, Uganda na Djibouti (kutoka Ukanda wa Mashariki), Cameroon, DRC na Equatorial Guinea (Kanda ya Kati), Afrika Kusini, Angola na Botswana (Kanda ya Kusini), Cote d’Ivoire, Gambia, Nigeria na Sierra Leone (Magharibi) na Misri na Morocco (Ukanda wa Kaskazini)".

"Nipende pia kuwataarifu kuwa pamoja na kuwa wajumbe, mwezi huu wa Mei 2024, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jukumu jingine kubwa zaidi,  tumeaminiwa kuwa Mwenyekiti wa baraza hili kwa mwezi Mei, hivyo, tukiwa wenyekiti tunalo jukumu kubwa la kusimamia shughuli zote zinahusu baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye bara la Afrika"

Aidha amesema katika kuelekea maadhimisho hayo Tanzania kwa kushirikiana na sekretarieti ya baraza hilo waliandaa ratiba ya shughuli mbalimbali ndani ya mwezi huo ambapo wiki ya kwanza itahusu usuluhishi na majadiliano, wiki ya pili ilihusu masuala ya mahitaji ya kibinadamu, amani na usalama, wiki ya tatu ilihusu wanawake na vijana katika amani na usalama na wiki ya nne ulinzi kwa watoto na wiki ya tano ilihusu kusaidia misheni za amani.

Amesema kuwa, miongoni mwa watu mashuhuri watakaoshiriki maadhimisho hayo ni Mhe. Jessica Alupo, Makamu Rais wa Uganda; Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Olesegun Obasanjo, Rais Mstaafu Burundi, Mhe. Domitien Ndayizeye, Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chissano na Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 

Aidha, katika kusherehekea Maadhimisho hayo, tarehe 24 Mei, 2024 kutafanyika mjadala wa wazi kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kupokea maoni yao kuhusu utendaji kazi wa baraza na namna ya kuweza kuliimarisha, kwani katika kipindi cha miaka 20 ya uhai wa baraza hilo limepata mafanikio katika kuimarisha amani na usalama Barani Afrika. 

"Kwa muktadha huo, nawakaribisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Mjadala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kutoa maoni yao, aidha, nawahimiza wadau wote walioalikwa kushiriki kwenye kilele cha maadhimisho tarehe 25 Mei 2024"amesema Waziri Makamba.

Katika hatua nyengine, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuimarisha diplomasia ya nchi na kuiongoza nchi katika kutoa kipaumbele kwenye masuala ya ulinzi na usalama katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla.  

Baraza la Amani na usalama ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi kuhusu masuala ya amani na usalama kwenye umoja wa Afrika, ambapo miongoni mwa majukumu ni pamoja na kuzuia kutokea kwa migogoro, kusuluhisha au kukabiliana nayo pale inapojitokeza na kutoa miongozo ya kushughulikia masuala ya kiusalama.


Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...