Skip to main content

DOYO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI ADC

 

Na Mwandishi wetu

Ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama chaAllience for Democratic Change, ADC,  Hamad Rashid kutangaza kuachia nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba, amejitokeza Katibu Mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan amesema amesema ameamua kuwania nafasi hiyo kutokana na uzoefu aliona ndani ya chama hicho ambapo atachukua fomu hiyo Jun 11 mwaka huu.

"Sababu kubwa ambayo imenifanya kuwania nafasi hii ni kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha baada ya kulelewa  vema na aliyekuwa Mwenyekiti wetu, Hamad Rashid.

Ameongeza "Nimekaa na Mwenyekiti wetu kwa muda wa miaka 10 nikiwa Katibu Mkuu na sikuwahi hata siku moja kutofautiana naye na nimejifunza mengi ikiwemo suala uvumilivu na kuheshimu Katiba, ambayo ameitekeleza kwa vitendo kwa kuondoka madarakanj kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea," amesema.

Amefafanua kuwa katika chama hicho ameweza kufanya kazi na viongozi mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa kwanza, Said Bilal huku Doyo akiwa Mkurugenzi wa Habari.

Pia amefanya kazi na Lucas Silimu aliyekuwa Katibu Mkuu wakati huo, Mama Lydia Bendera (Katibu Mkuu), Juma Kilagai (Katibu Mkuu) na Abubakari Rakesh.

Aidha, amewataka wanachama wa chama hicho kutokuwa na wasiwasi naye katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Juni 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa ikiwa atafanikiwa kushika nafasi hiyo, moja ya mikakati yake ni kukiimarisha chama kiwe kikuu cha upinzani na kifanye vizuri bungeni na kuisimamia vema Serikali maslahi ya Watanzania.

Amesema kuwa, ikiwa atafanikiwa kukaa katika kiti hicho atabeba agenda tatu ambazo ni mabadiliko ya sheria, mabadiliko ya ajira ambayo itafanya wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia maishani na agenda ya maisha bora kwa mtanzania.

Aidha, akitangaza kuwania nafasi hiyo aliambatana na  anayegombea umakamu uenyekiti, Scolastica Kahana aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Kibaha Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Hata hivyo, ametoa wito kwa wana siasa ambao wameshindwa kwenye chaguzi wa ndani ya vyama kujiunga na ADC ili kuongeza nguvu ya kufanya vema kwenye chaguzi, zijazowa Serikali za Mitaa Oktoba mwaka huu na uchaguzi Mkuu utakaofanyika  mwakani.

"Ni vizuri hata ndg yetu Peter Msigwa ambaye amshindwa kwenye uchaguzi wa ndani wa  chama, kama itampendeza anaweza kujiunga kwetu na ninaaminj attuingezea nguvu kubwa kwenye ushindani wa siasa ya vyama vingi," amesema.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...