Skip to main content

FRIENDS OF SERENGETI YATOA UFADHILI WA VIFAA VYA DORIA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA TZS. MILLIONI 40 KWA ASKARI WA UHIFADHI WA TAWA


Na Beatus Maganja, Arusha.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhifadhi na kulinda rasilimali za wanyamapori nchini ikiwa ni pamoja na  kudhibiti wa wanyama wakali na waharibifu,  Marafiki wa Serengeti Uswisi "Friends of Serengeti Switzerland" wametoa msaada wa mahema 20, mabegi ya kulalia "Sleeping bags" 20 yenye  thamani ya Shillingi Millioni thelathini laki tisa na elfu arobaini (30,940,000/=) pamoja na Lita 2,120 za mafuta ya gari zenye thamani ya Shillingi Millioni Saba (7,000,000/=) kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria kwa Askari wa TAWA Kanda ya Kaskazini.

Akimkabidhi Kaimu Kamanda wa Uhifadhi TAWA Kanda ya Kaskazini Privatus Kasisi msaada huo Katika Ofisi za Kanda zilizopo jijini Arusha Juni 09, 2024, Bi Suzan Peter Shio Kwa niaba ya bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi amesema lengo na shabaha yao ni kusimamia uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ili kuhakikisha Tanzania inakuwa katika hali yake ya uasili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

"Tumekuwa tukifanya shughuli za ufadhili wa uhifadhi kwa miaka kadhaa nchini Tanzania, na kwa TAWA tumeanza zaidi ya miaka 10 iliyopita (tangu ikiwa Idara ya Wanyamapori) na  hasa tulijikita kwenye ufadhili wa mafuta kwa ajili ya kuwasaidia Askari kufanya doria" amesema

Aidha Bi Suzan ameishukuru TAWA kwa ushirikiano inayoendelea kuutoa kwa wadau hao na kukiri kuwa ushirikiano huo umekuwa chachu ya kuwapa moyo wa kuendelea kuwafadhili.

Naye Kaimu Kamanda wa Uhifadhi TAWA Kanda ya Kaskazini Privatus Kasisi ameishukuru bodi ya Marafiki wa Serengeti kwa ufadhili huo ambao unalenga kuboresha  usimamizi wa shughuli za uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori hususani katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu katika Kanda yake anayoisimamia.

"Sisi kama TAWA tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi ambao wamekuwa wakitusaidia misaada mbalimbali kwa ajili ya kusimamia uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori kwa muda mrefu na wamekuwa wakitupa mafuta, mahema na viona mbali "binoculars" amesema

Amesema Kanda ya Kaskazini inasimamia maeneo makubwa ambayo ni mikoa minne ya Manyara, Arusha, Tanga na Kilimanjaro ambayo yamekuwa yanakumbwa na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hivyo kwa kupatiwa msaada huo hususani mahema yatawasaidia sana Askari kufanya kazi zao ipasavyo hasa kwa kazi za dharura zinazojitokeza mara kwa mara na kuwalazimu kwenda maeneo ambayo hayana vituo vya kudumu vya Askari.

Vilevile, ameiomba bodi hiyo kuendelea kuisaidia TAWA hususani Kanda hiyo kwakuwa wanasimamia maeneo makubwa yenye changamoto kubwa ya wanyamapori wakali na waharibifu na uhitaji bado ni mkubwa

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...