Skip to main content

MKANDARASI ATAKIWA KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA JUA KISHAPU




picha mbalimbali za matukio 

*Amtaka Meneja kuhakikisha  anawasimamia vema mkandarasi

*Mradi kuleta tija kwenye upatikanaji wa Umeme 

Kishapu, Shinyanga

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga ameridhishwa na hatua mbalimbali za maendeleo katika upatikanaji wa huduma ya Umeme mkoani  Shinyanga huku akimsisitiza mkandarasi mradi wa umeme wa Jua wilaya ya Kishapu kukamilisha mradi huo kwa wakati utakaozalisha Megawati 150.

Kamishna Luoga amempongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na menejimenti yake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya umeme huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati miradi inayoendelea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali

 "Nikupongeze meneja kwa usimamizi mzuri kwa wakandarasi maana ukimsimamia hawezi kuacha kufanya kazi ,mara nyingi sana wakandarasi wanazembea au wanakimbia ni kwa sababu tu haupo usimamizi mzuri kwahiyo ongezeni usimamizi kwa hao wakandarasi ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi na kufanya nao vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto na maendeleo ya miradi," Alisisitiza Mha. Luoga

Kuhusu masuala ya usimamizi kwenye miundombinu na uharibifu unaofanyika Mha. Luoga alisema ,wale wanaofanya kwa makusudi au kwa kutokujua wanapaswa kupatiwa elimu kuhusu athari za uharibifu wa miundo mbinu hiyo na namna ya kuilinda.

Alisisitiza kuwa mradi huo wa umeme wa Jua  ni muhimu sana kwani mara baada ya kukamilika utaongeza kiasi cha uzalishaji umeme nchini pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Pia, aliwataka wakandarasi kuhakikisha hawacheleweshi utekelezaji wa mradi wa Jua wa Kishapu na waukamilishe kwa ubora wa hali ya juu na kuongeza kuwa kipaumbele cha ajira kitolewe kwa wanawake.

Awali, akisoma taarifa ya miradi ya kusambaza umeme kwa mwaka wa fedha 2023/2024 meneja wa shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe alisema, mradi wa umeme wa jua unaotekelezwa katika maeneo ya Ngunga Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia kumi (10) ambapo unatarajiwa kukamilika Mwezi Februari 2025.

“Hali ya usambazaji Umeme imeendelea kuimarika kutokana na miradi mbalimbali ya kusambaza Umeme inayotekelezwa na TANESCO na ile ya kusambaza Umeme vijijini inayofadhiliwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA)”.

Kamishna Luoga alikagua pia mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli pamoja na mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Ibadakuli hadi Simiyu 

Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga  Mha. Leo Mwakatobe pamoja na mambo mengine amesema shirika hilo linasimamia miradi miwili (2) ya kimkakati ambayo ni mradi wa Umeme wa Jua Wilaya ya Kishapu pamoja na mradi wa kuboresha upatikanaji Umeme Bulyanhulu ikiwa lengo ni kuongeza uzalisha Umeme na kuboresha upatikanaji Umeme.

“Mradi wa Umeme wa Jua, kutokana na mahitaji ya Umeme kuongezeka serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Umeme Jua maeneo ya Ngunga Kishapu ili kuongeza kiwango cha upatikanaji Umeme Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine ya Nchi, mradi huu unatarajiwa kuzalisha Umeme wa kiasi cha Megawati 150 ambapo mradi unathamani ya ya zaidi ya bilioni 300 na umegawanyika katika awamu mbili ya kwanza ni MW 50 na mkandarasi ni SINOHYDRO ambapo mkandarasi ameshakabidhiwa kazi na kuanza ujenzi Mwezi Oktoba 2023, na kwa sasa mradi upo asilimia 10 na matarajio ya kukamilika ni baada ya Miezi kumi na nne (14).

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...