Skip to main content

BUKOMBE WAISHUKURU SERIKALI KWA MAENDELEO

#Wajivunia ujenzi wa miundombinu huduma za jamii.

#Dkt. Biteko Asisitiza umuhimu wa ushirikiano kuleta maendeleo.

#Ataka Wananchi kuchagua Viongozi Wenye Sifa


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyowapa Watu wa Bukombe kwa kuwaletea Maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa wa hadhara katika Uwanja wa Lyambamgongo Center iliyopo Kata ya Lyambamgongo, Jimbo la Bukombe mkoani Geita.

“ Nataka niwambieni mambo mazuri yanakuja, Mama Samia amesema anataka aione Bukombe mpya na mimi nawahakikishieni itabadilika Lyambamgongo haikuwa hivi na ninyi ni mashahidi lakini Rais wetu ametuletea huduma mbalimbali za maendeleo na leo tumepata barabara ya kutoka Lyambamgongo hadi Ifunde, Ishoro, Nyamakungu, hatukuwa na Zahanati leo tumepata Zahanati na Nishati ya umeme wa uhakika mambo mazuri zaidi yanakuja na Bukombe itabadilika”. amesisitiza Dkt. Biteko.

Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wa Kijiji cha Lyambamgongo na Jimbo la Bukombe kwa ujumla kujiandaa kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu kwa kuchagua viongozi wenye sifa watakaosaidia kuleta maendeleo.

“ Muda utakapofika tuwe tayari kwaajili ya kujiandikisha katika Daftari la kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi wazuri wenye sifa za kuchaguliwa ambao watasaidia kuleta maendeleo, tunataka jimbo la Bukombe libadilike kwa kuwa na watu wenye maono au mawazo mazuri yatakayosaidia utatuzi wa changamoto zinazotukabili”, amefafanua na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara mkoani Geita na kuwasalimia wa Bukombe kwa kuwa anataka kuona miradi mingi inatekelezwa na hivyo yeye kama Mbunge ataendelea  kuhakikisha maendeleo ya kweli yanaenda kwenye maeneo ya wananchi.

Naye, Diwani wa kata ya Lyambamgongo, Mhe. Bonifasi Shitobelo amesema hapo awali huduma zilikuwa mbali na gharama za kwenda kupata matibabu zilikuwa juu lakini sasa Serikali imesogeza huduma kwa wananchi.

Tunaishukuru serkali na mbunge wetu Mhe. Doto Biteko kwa kuwezesha ukamirishaji wa ujenzi wa Zahanati, Barabara ya kutoka Lyambamgongo hadi Ifunde na Shule ya Msingi katika jimbo la Bukombe.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Bw. Nicholaus Kasendamila amemshukuru Dkt. Biteko kwa kuendelea kuwasaidia wananchi wa Bukombe kwa kuhakikisha wanapata maendeleo kwa kuwa na miradi mbalimbali

Aidha, amewasihi wananchi wa Bukombe kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa “Huu  ni mwaka wa uchaguzi  tunatakiwa kujiandaa  na viongozi wa CCM katika Mkoa huo tuhamasishe wapiga kura kushiriki katika uchaguzi na hatimaye kuchagua viongozi  wazuri”.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Mhe. Stanslaus Nyongo amesema kuwa Mbunge anaefanya kazi vizuri anatangaza Jimbo łake na leo hii Dkt. Doto Biteko ameendelea kulitangaza vema jambo hilo kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo la Bukombe.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...