Skip to main content

KAMPENI YA KILIMO NI MBOLEA KUCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA, USAJILI WA WAKULIMA.

 




Na Mwandishi wetu, Ruvuma.

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema matumizi sahihi ya mbolea katika uzalishaji wa mazao ni muhimu kwa lengo la kurutubisha na kuboresha afya ya udongo ili kuweza kuzalisha mazao kwa wingi kati eneo dogo. 

Kauli hiyo imetolewa Wilayani Mbinga na Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Joele Laurent alipozungumza na kusanyiko la wakulima wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya TFRA ijulikanayo kwa jina la KILIMO NI MBOLEA, yenye lengo la kuhimiza matumizi sahihi ya Mbolea na kuhamasisha wakulima kujisajili na kuuhisha taarifa zao kwenye mfumo wa Mbolea ya ruzuku, ili waendelee kunufaika na mpango huo.

Mkurugenzi huyo amesema, idadi ya watu inaongezeka kila kukicha hivyo matumizi sahihi ya mbolea shambani ni muhimu ili kuongeza tija na kutosheleza mahitaji ya chakula kukidhi idadi ya watu iliyopo.

Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ukuaji wa miji, miundombinu na huduma nyingine za kijamii unapunguza eneo linalofaa kwa kilimo na hivyo eneo linalobaki linatakiwa kutumika kwa ufanisi kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea kwa kuongeza tija.

Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, kuongeza tija ya uzalishaji kupitia matumizi sahihi ya mbolea kunachangia kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja, ukuaji wa Sekta ya Kilimo na pato la taifa kwa ujumla, hivyo ni matarajio ya TFRA kuwa kupitia kampeni ya KILIMO NI MBOLEA wakulima watanufaika katika shughuli zao za kilimo kwa ujumla.

‘‘Kampeni hii ni muhimu kwa wakulima wote wakati huu tukielekea kwenye msimu wa kilimo wa mwaka 2024/2025, matarajio yetu ni kwamba hamasa ya usajili wa wakulima kwenye mfumo wa mbolea ya ruzuku itaongezeka na hivyo wakulima kunufaika na mpango wa mbolea ya ruzuku na kuongeza tija baada ya kuitumia mbolea hiyo kwa usahihi’’, alisema Mkuruugenzi huyo.

Akielezea hali ya matumizi ya mbolea nchini Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa matumizi yameongezeka kutoka tani 363,599 katika msimu wa 2021/22  hadi kufikia tani 840,714 katika msimu 2023/24. Huku akiutaja mkoa wa ruvuma kuwa ni moja ya Mikoa ya Kimkakati ya uzalishaji wa chakula nchini kwa miaka ya hivi karibuni na unaongoza kwa matumizi ya mbolea.

‘‘Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/23 Mkoa wa Ruvuma ulitumia kiasi cha tani 83,472 ukifuatiwa na Mikoa ya Njombe tani 75,358, Mbeya tani 75,252, Songwe  tani 71,230  na  Mkoa wa Iringa tani 44,214 hii ni mikoa yenye matumizi makubwa ya  mbolea nchini. Kwa mwaka 2023/24 Mkoa wa Ruvuma umetumia tani 113,000 za mbolea na kufanya Mkoa huu kuwa ni miongoni mwa Mikoa tegemezi katika uzalishaji wa chakula’’, alibainisha Mkurugenzi huyo.

Nae Mkurugenzi wa uzalishaji wa ndani na uagizaji wa mbolea kwa pamoja wa mamlaka hiyo Louis Kasera, amesema ili wakulima waweze kunufaika na Mbolea ni vema waende kujisajili kwenye mfumo wa mbolea ya ruzuku na wakulima waliojiandikisha waende kuuhisha taarifa zao. 

Kwaupande wake balozi wa kampeni ya KILIMO NI MBOLEA Abdallah Nzunda maarufu Mkojani aliwasisitizia wakulima kutoa ushirikiano wakati wa kampeni na  baada ya kampeni ili waendelee kunufaika na elimu inayotolewa ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa mbolea ya ruzuku.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga Wilayani Mbinga, nakuhudhuriwa na wakulima zaidi ya 1500 kutoka maeneo mbalimbali ya Mbinga, viongozi wa Sekretarieti za Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Mbinga, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini,  na baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya Mbolea, ambapo kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo wakulima walipata elimu ya matumizi sahihi ya mbolea na matumizi ya chokaa kilimo.

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...