Skip to main content

NAIBU WAZIRI MKUU DKT BITEKO MGENI RASMI UZINDUZI WA SERA YA TAIFA BIASHARA 2003 TOLEO LA 2023

 

Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Seleman Jafo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio yaliopatikana katika sera ya taifa ya biashara mwaka 2003 toleo la 2023 ni Serikali kufanikiwa kushiriki kikamilifu katika majadiliano mbalimbali ya biashara baina ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa kwa lengo la kuongeza fursa zaidi za biashara ya bidhaa na huduma kutoka Tanzania ikijumuisha kupata masoko yenye masharti nafuu kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania.

Akizungumza na waandiahi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Tanzania imefika mauzo ya nje Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika yameongezeka kutoka shilingi trilioni 2.607 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 4.422 mwaka 2023, na mauzo nje kwenye Jumuiya ya Ulaya yameongezeka kutoka shilingi trilioni 0.605 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 3.835.65 mwaka 2023, huku bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni za kilimo, hususan kahawa, chai, mahindi, ngano, mchele, mbogamboga na bidhaa za viwandani.

Amesema kuwa, Serikali imefanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Biashara ya mwaka 2003 na kutoa toleo la 2023, lenye lengo la kuweka mfumo mkakati madhubuti unaolenga kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza ukuaji wa kiuchumi na kuboresha ustawi wa wananchi na utekelezaji wa sera hiyo utailetea nchi faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mchango wa sekta ya biashara katika pato la taifa.

Sera hiyo mpya inalenga kuimarisha na kuendeleza biashara ya ndani na nje, pamoja na kuimarisha mtengamano na ushiriki wa nchi katika biashara na nchi zingine rafiki, kikanda na kimataifa.

“Sera hii ni marejeo ya sera ya mwaka 2003 ambayo imefanyiwa marekebisho ili iweze kuendana na mabadiliko ambayo yametokea katika nyanja mbalimbali kikanda na kimataifa,” amesema Dkt Jafo.

Sanjari na hayo ameongeza kuwa sera hiyo  itaimarisha mazingira ya ufanyaji biashara, kuvutia uwekezaji, kuongeza shughuli za biashara na ajira, kuongeza kipato cha wananchi, na kuimarika kwa uzalishaji viwandani kutokana na upatikanaji wa masoko ya uhakika hivyo kuchochea jitihada za ujenzi wa uchumi wa viwanda.

"Sera hii inaongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Ushindani wa Biashara katika kuchochea kasi ya Mabadiliko ya Kijamii na Kiuchumi yanayoongozwa na Viwanda’. Inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumanne, Julai 30 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Mashaka Biteko," amesema Dkt Jafo.

Dkt Jafo amebainisha  kuwa sera hiyo itachangia kuwepo kwa ushindani huru na haki katika biashara, kumlinda mlaji, kuimarika kwa ratibu wa biashara, na kuondokana na mgongano wa kisera, kisheria, na mgawanyo wa majukumu ya kitaasisi katika masuala ya biashara.

"Kuimarika kwa miundombinu ya masoko na biashara; kuimarika na kuongezeka kwa biashara ya nje, na kuongezeka kwa ufanisi katika utendaji wa shughuli za biashara kupitia matumizi ya mifumo ya kibiashara,"amesema " Waziri Jafo.

Waziri Jafo ametaja baadhi ya mambo yaliyoainishwa katika sera hiyo ni kuimarisha, kukuza na kuendeleza biashara ya ndani na nje, kuimarisha mtengamano na ushiriki wa nchi katika biashara na nchi zingine rafiki, kikanda na kimataifa, na kuimarisha maendeleo na ujenzi wa miundombinu ya masoko na biashara.

Amesema sera hiyo pia melenga kuimarisha usimamizi wa ushindani halali wa kibiashara na kumlinda mlaji, kuendeleza biashara ya huduma, kuwezesha na kuimarisha biashara mtandao kupitia matumizi ya teknolojia, na kuimarisha na  upatikanaji wa mikopo na mitaji ya biashara.

"Fursa hizi ni pamoja na zile zinazotokana na soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), AfCFTA, soko la China kwa kuuza bidhaa bila kulipa ushuru wala kikomo kwa asilimia 98 ya bidhaa zote kutoka Tanzania, India, AGOA kwa kuuza zaidi ya bidhaa 6,400 bila ushuru" amesema  

Dkt Jafo.

Ameongeza kuwa, faida nyingine ni kumewezesha mchango wa biashara katika pato la taifa kufikia asilimia 8.3 mwaka 2023, kupitia fursa hizo mauzo kwenda Jumuiya ya Afrika Mashariki yameongezeka kutoka shilingi trilioni 1.12 mwaka 2016 hadi Sh trilioni 3.022 kwa mwaka huo.

Hata hivyo, amesema mauzo ya nje kwenye Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika yameongezeka kutoka shilingi trilioni 2.607 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 4.422 mwaka 2023, na mauzo nje kwenye Jumuiya ya Ulaya yameongezeka kutoka shilingi trilioni 0.605 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 3.835.65 mwaka 2023, huku bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni za kilimo, hususan kahawa, chai, mahindi, ngano, mchele, mbogamboga na bidhaa za viwandani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Trade Mark Afrika, Elibariki Shami, aliipongeza Tanzania kwa kufanya maboresho hayo na kusisitiza kuwa ni vema kila taifa liige hatua hiyo ili biashara ziweze kufanyika kwa urahisi.

"Sera hii itarahisisha kufanya biashara katika maeneo mbalimbali ya kikanda kwa sababu nchi nyingi za Afrika zinashindwa kufanya kwa pamoja kwa sababu ya kukinzana katika sera za biashara" amesema Shami.

Aidha Julai ,30,2024 Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa nishati  Dkt Doto Biteko anatarajiwa kuhudhuria katika hafla ya uzinduzi wa sera ya Taifa biashara 2003 toleo la 2023   itakayofanyika katika ukumbia wa Mlimani city Jijini Dar es salaam

Comments

Popular posts from this blog

MWAKIPOSA MWENYEKITI MPYA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA DAR

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Boko Wilaya ya Kinondoni, Razalous Mwakiposa ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam kwa kupata kura 24 kati ya 37 zilizopigwa na wajumbe mapema leo hii. Uchaguzi huo umemalizika leo June 20, 2026ambapo  ulikua unahusisha nafasi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu, ambapo Mwenyekiti ameshinda Razalous Mwakiposa huku Katibu Mkuu akiwa ni Peppino Sudi Peppino . Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi, Kambi Sinde, amesema kuwa Razalous Mwakiposa ameshinda kwa kupata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akishinda kwa kura 20 kati ya kura 37 zilizopigwa. "Uchaguzi umefanyika kwa uwazi na haki, kulikuwa na jumla ya wajumbe 40, lakini watatu walipata udhuru, hivyo, leo waliopiga kura ni wajumbe 37 na matokeo ni kwamba mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti amepata kura 24 kati ya kura 37 zilizopigwa, huku Katibu Mkuu akipata kura 20 kati ya kura 37 zilizop...

TIRDO YAVUNJA VIKWAZO VYA UBUNIFU, AFRO HEAL YAGEUZA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

Na Ayra News.  Mashauri Enock Shushu, kutoka Afro heal Group Limited, amesema malezi ya ubunifu kupitia shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) yameiwezeshaa kampuni hiyo kubadili dawa za asili zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia magome ya miti na kuzigeuza kuwa bidhaa za kisasa zinazokidhi viwango vya ubora na mahitaji utengenezaji soko. Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane 2026, Shushu alisema Afro healGroup Limited ni kampuni inayojihusisha na utafiti na utengenezaji wa dawa za binadamu zinazotokana na mimea ya asili, huku TIRDO ikiwa imekuwa nguzo muhimu katika kukuza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji. Alisema kabla ya kujiunga na TIRDO, kampuni hiyo ilikuwa ikitengeneza dawa za asili katika mfumo wa magome, lakini baada ya kupata malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na uwekezaji wa rasilimali watu kupitia taasisi hiyo, imefanikiwa kuziboresha na kuzalisha bidhaa za kisasa zinazorahisisha matumizi kwa wananchi. Shushu alisema ushirikiano kati ya wa...

VETA KAGERA WABUNI MTEGO KISASA WA KUVUNA SENENE

Ayra Nwestz  Chuo cha Veta mkoa wa Kagera VTC kimebuni mtambo wa kisasa wa kuvuna senene ambao unamuwezesha mvunaji kunapata senene wengi kwa wakati mmoja ambao wanakua salama. Akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima, katika maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa, Mwalimu wa Kagera VTC, Elias Lucas Mayala, amesema chuo hicho kimebuni mtego huo una lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na mbinu za jadi za uvunaji. Mayala amesema kuwa mtanbo huo una uwezo wa kubeba kati ya kilo 80 hadi 100 za senene kwa wakati mmoja wakati wa uvunaji.  Aidha, amesema mtego huo una mfumo wa kuchuja senene wanapoingia na kuwatenganisha wadudu wadogo wadogo, ambao wanaweza kutumika kama chakula cha kuku badala ya kutupwa. Ameeleza kuwa tofauti na mbinu za zamani zinazoweza kuharibu miti na mazalia ya senene, mtego huo ni rafiki wa mazingira na umeundwa kwa namna inayorahisisha matumizi yake, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kusogezwa kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na mahitaji...